KUTOKA SAUT-MWANZA MDAHALO WA KATIBA MPYA.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  kwa kushirikiana na Chuo cha Mtakatifu Agustino-Mwanza limefanya mdahalo wa wazi juu ya mchakato mzima wa katiba mpya kwa wananchi wote katika Chuo hicho hapo Mwanza. Huu ni mwendelezo wa midahalo inayofanywa na kituo hicho sehemu mbalimbali ya nchi baada ya ile iliyofanyika Dar es salaam na Zanzibar. Mgeni Rasmi katika mdahalo huo ambao ilihudhuriwa na Wanafunzi, wanaharakati na wananchi mbalimbali kutoka jiji la mwanza alikuwa ni Prof. Chris Maina kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambae pia alikuwa mtoa mada mkuu, Makamu mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino Rev. Dr. Charles Kitima alikuwa ni mgeni mualikwa . Mchokoza mada alikuwa ni Dr. Makulilo na takribani ya watu elfu moja walihudhuria ambapo watu thelathini na moja walichangia mada katika Mdahalo huu.

Maandalizi ya urushaji wa matangazo kabla ya tukio usiku wa kuamkia jumamosi, mdahalo ulirushwa moja kwa moja na startv.

Wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wakiingia katika ukumbi wa M13 SAUT-MWANZA.

Wadau wakiingia ukumbini tayari kusikiliza na kuchangia mdahalo.

Mdau na mpiganaji Mwanahapa Izack mwanafunzi wa mwaka wa tatu shahada ya Mahusiano ya Jamii na Masoko akiwa tayari ukumbini kusikiliza mdahalo kabla ya kuanza.

Wadau wa shahada ya Mahusiano ya Jamii na Masoko wakiwa wanafuatilia mdahalo huo.

Meza kuu nayo ilikuwa ikifuatili kwa makini mawazo na michango ya wachangiaji mbalimbali katika mdahalo huo, watatu kutoka kushoto ni mgeni rasmi na makamu mkuu wa SAUT Rev. Dr. Kitima pamoja na Prof. Maina Kutoka UDSM anaefuatia.

Mwenyekiti wa mdahalo huo akichagua mchangia mada hayupo pichani kwa ajili ya kutoa maoni yake.

Mchokoza mada wa mdahalo huu Prof. Maina kutoka UDSM akichokoza baadhi ya mambo mbalimbali kutoka katika katiba ya sasa huku yeye akitoa vifungu vinavyogongana kwenye katiba mbili ya Zanzibar na Tanzania huku akisema mgongano huo unaotokana na matatizo ya Kisiasa na kitaalamu.

Mgeni Rasmi na makamu mkuu wa chuo cha Mtakatifu Agustino Rev. Dr. Charles Kitima akisema jambo katika mdahalo huo wa mchakato wa katiba mpya.Umma wa Wanafunzi mbalimbali na wananchi kutoka jijini Mwanza wakisikiliza kwa makini mdahalo huo.

Sister nae alikuwa mchangiaji katika mchakato mzima wa kuandwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwanzafunzi wa SAUT bi khadija Ramadhani kutoka Zanzibar akichangia mchango wake. Alieleza jinsi gani anavyosikitishwa kuona Rais wa Zanzibar akiwa Bungeni hapewi nafasi sawa ya heshima kama apewayo Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania pia alisisitizia uwepo wa marais watatu yani wa Tanganyika, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Askofu Yohana Kutoka kanisa la CCCT Mwanza akiwa ni mmoja ya mchangiaji katika mdahalo huo kwa kuzingatia mdahalo ulitoa fursa ya wawakilishi wa kada mbalimbali kutoa maoni yao.

Mwanafunzi kutoka SAUT shahada ya Uwalimu akitoa maoni yake. Huyu aliacha maswali ambayo yalitoa changamoto wa washiriki wengine pale aliposema "Muungano wa Zanzibar ulitokana na kuungana kwa vyama vya TANU na ASP na kuunda CCM, je CCM ikitoka madarakani na chama kingine kuchukua madaraka Muungano huu utakuwepo au nao utaondoka?, Au CCM itatawala milele?"

Bw. Kulwa Machela muwakilishi kutoka chama cha wavuvi mkoani Mwanza akichangia mada katika mdahalo huo, alisema katika katiba swala la umiliki wa Ardhi lizingatiwe na ikiwezekana kila mwananchi apewe kipande chake, pia aliendelea kuhoji kwanini Mkulima hana pensheni kama wafanyakazi wengine, akaongeza kuwa hela ya kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo ya shilingi elfu saba na mia tano haiwatoshi kwani maisha ya sasa yameshabadilika hivyo kuitaka serikali kuongeza pesa, ambapo aliacha wanafunzi wakimshangilia kwa dakika kadhaa.

Grace Lyoba Mwananchi kutoka kijiji cha Luchelele kinachopakana na mipaka ya chuo cha Mt. Agustino akichangia mawazo yake ambapo alianza kwa kusema kwamba ndo kwa mara yake ya kwanza kuiona katiba ya nchi yake kwani alikuwa hajui hata rangi ya katiba na kusema "Kumbe ina rangi ya zambarau" na kuwaacha washiriki wakicheka, pia alitaka katiba mpya kuzingatia utut wa mwanamke.

Katibu wa YUNA tawi la SAUT Mr. Malisa Godlisten akichangia katika mdahalo huo.

Ndugu Chacha Marwa kutoka Open University of Tanzania akichangia mada katika mdahalo huo.

Bi. Consolatha Mosha mwanafunzi wa mwaka wa Pili fani ya Uwalimu kutoka SAUT akichangia maoni yake pia katika mdahalo huo.

Makamu mkuu wa chuo, mchokoza mada pamoja na Mkuu wa kitivo cha sheria SAUT wakiongea jambo mara baada ya kumalizika kwa mdahalo huo leo.

Advertisements

One response to “KUTOKA SAUT-MWANZA MDAHALO WA KATIBA MPYA.

 1. Will all these effort put by Tanzanians put into action or its the the matter of time?
  I will leave these questions……
  1. Why do Tanzanian need a new constitution?
  2. What problems do Tanzanians face to demand a new constitution?
  3.What effect will people get if the constitution will not be changed?
  4. What difference will it make if we have a new constitution with the same political party in leading the country?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s