KUTOKA CBE MWANZA-STUDENTS FAMILY DAY PARTY YAFANA HUKO LAVENA BEACH.

Uongozi wa serikali ya wanafunzi katika Chuo cha Elimu ya Biashara (COBESO) tawi la Mwanza na wanafunzi wa chuo hicho wafanya sherehe ya pamoja na katika kusheherekea mwanzo mpya wa masomo huku wakipata Mr. and Miss CBE-Mwanza kwa mwaka 2011/2012 baada ya mchuano mkali ulifanyika katika fukwe za Lavena luchelele karibu na chuo cha Mt. Augustino jijini mwanza. Kwa upande wa Mr. CBE-Mwanza 2011/2012 mshindi alikuwa ni Ally Thabit aliyejinyakulia zawadi ya Jiko la Umeme la plate mbili, saa ya ukutani, moderm kutoka Zantel pamoja na elfu thelathini pesa taslimu, kwa upande wa Miss CBE-Mwanza 2011/2012 mshindi alikuwa ni Happy Dash aliyejinyakulia Jiko la umeme lenye plate mbili, saa ya ukutani, moderm kutoka Zantel na elfu thelathini pesa taslimu.

Pata matukio katika picha kujionea kilichojiri…

Viongozi wa ngazi mbalimbali wa COBESO wakiwa tayari kushuhudia mchuano wa Miss and Mr. CBE tawi la Mwanza 2011/2012.Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Elimu ya Biashara tawi la mwanza (COBESO) katikati akiwa na Katibu wake mkuu kushoto.Majaji wa shindano la kumpata Mr. and Miss CBE-Mwanza wakiwa tayari kwa ajili ya kufanya kazi yao.DJ akiwa full mzuka on turntable katika kudondosha ngoma kali kwenye party hiyo. This DJ is from the Stone Club jijini Mwanza.Hapa ilikuwa ni katika kajifoleni cha kwenda kupata msosi ulioandaliwa na COBESO.

Warembo pamoja na washikaji wakila pozi juu ya jiwe ilimradi tu kutaka kuona na kujua nini kinajiri katika fukwe hizo za Lavena.

Wadau kutoka chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) wakiwa pamoja katika kuwapa kampany washkaji zao wa CBE na kuonyesha ushirikiano wa kutosha pande izo .

Huku wengine walikuwa katika kajifoleni cha kwenda kupanda msosi.

Luk on there Swaga..Warembo wa mwaka wa kwanza toka CBE wakiwa katika pozi pande hizo.

Mdau kutoka CocaCola Mwanza Mr. Ruta akiwa katika pozi lake. CocaCola walikuwa ni wadhamini wa party hiyo kwa upande wa vinywaji.

HAHAHAHAHAH..Haikuwa ugomvi kama unavyoweza kudhani bali ilikuwa tu moja kati ya sehemu ya burudani..Wote hao walikuwa wakihangaika kwa ajili ya kupata complimentary za kuingilia Villa Club ya Mwanza ili mradi tu kuweza kuendeleza bata zilizoanza toka mishale ya asubuhi.

Don mkubwa sana pande za CBE akila swaga za kutosha na mrembo pande izo.

Ilikuwa ni "Twende kushoto sho twende kulia ku twende kushoto sho twende kulia ku" yani fu kisauzi pande zile pale..DaaaahHapo twende...izo zote ni katika kusherehekea tu kwa pamoja kwenye boje moja la party pande za Lavena Beach.

Ebwana ndiooooooo...

WASHIRIKI WA MISS AND MR. CBE-MWANZA 2011/2012 WAKIENDA JUKWAANI.

Mshindi wa Miss CBE 2011/2012 Miss Happy Dash na Mshiriki namba sita katika upande wa kumtafuta Mr. CBE wakiwa katika pozi wakionyesha ujuzi wao jukwaani.

Mshiriki wa Umiss Mary Anga nae akionyesha swaga zake jukwaani.

Ilikuwa ni full kuonyesheana maujuzi ya kiumiss na kiu Mr. pale jukwaani.

Mr. CBE 2011/2012 Ally Thabit akionyesha mambo yake kabla ya kutangazwa kuwa mshindi akiwa na Mshiriki Umiss namba 2 Elizabeth Ezrael katika pozi za kimiss ambae yeye alikuwa mshindi wa Tatu Miss CBE 2011/2012 .

Mshindi wa Tatu katika shindano la Mr. CBE-Mwanza 2011/2012 Hilary Amos ambaye alijinyakulia jiko la umeme la plate moja na shilingi elfu kumi taslimu.

Mshindi wa Pili wa shindano la Mr. CBE-Mwanza 2011/2012 Laurian Julius akipongezwa na mrembo, yeye alijinyakulia jiko la umeme la plate moja, saa ya ukutani pamoja na fedha taslimu shilingi elfu ishirini.

MR.CBE-MWANZA 2011/2012 AKIPONGEZWA NA MASHABIKI WAKE BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI NA JAJI MKUU KATIKA MASHINDANO HAYO. YEYE ALIPATA JIKO LENYE LA UMEME LA PLATE MBILI, SAA YA UKUTANI, MODERM YA ZANTEL PAMOJA NA FEDHA TASLIMU SHILINGI ELFU THELATHINI.

Mshindi wa tatu wa miss CBE 2011/2012 MWANZA miss Elizabeth Ezrael akienda kuchukua zawadi ya jiko la umeme la plate moja pamoja na fedha taslimu elfu kumi.

Miss namba mbili Miranga Sosy Miranga Sosy akikabodhiwa zawadi zake ambazo ni jiko la umeme la plate moja, saa ya ukutani na fedha taslimu shilingi elfu kumi.

MISS CBE-MWANZA 2011/2012 HAPPY DASH AKIKUMBATIANA NA RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI CBE MWANZA BAADA YA KUTANGAZWA KUWA MSHINDI. ALIJINYAKULIA JIKO LA UMEME LA PLATE MBILI, SAA YA UKUTANI TOKA COCACOLA, MODERM TOKA ZANTEL PAMOJA NA FEDHA TASLIMU ALFU THELATHINI.

Hii ilikuwa ni baada ya kwisha kwa sherehe wadau walikuwa wakisubiria usafiri wa kuwarudisha mmakwao baada ya kumalizika kwa party.

Wadau walikuwa ni wengi sana wakisubiria usafiri.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s