TIMU YA SOKA YA SAUT YAANZA MAZOEZI KUJIANDA NA MECHI ZA KIRAFIKI DHIDI YA BUGANDO NA TOTO AFRICA.

Timu ya mpira wa miguu ya SAUT-Mwanza inafanya mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kujiweka vizuri kabla ya kucheza mechi mbili za kirafiki zinazotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii. Mechi ya kwanza inatarajiwa kuwa ni dhidi ya Toto Africa ya jijini Mwanza timu ambayo inashiriki katika Ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania bara mechi ambayo inatarajiwa kuwa kati ya Alhamisi na Ijumaa ya wiki hii katika uwanja wa CCM kirumba lakini hakuna taarifa za uhakika zenye kuthibitisha siku na uwanja utakaotumiwa. Mechi ya pili ni ile kati ya SAUT na na Chuo kikuu cha Tiba cha Bugando mechi ambayo itachezwa katika uwanja wa Nyamagana katika sherehe za kuzindua rasmi chuo cha Bugando kwa kuwa chuo rasmi kinachojitegemea.

Timu ya soka ya SAUT-MWANZA ikijifua kwenye uwanja wa Raila Odinga chuoni hapo.

Kocha mkuu akifundisha kwa vitendo uwanjani (mwenye track nyeupe).

Baadhi ya wachezaji wakiwa kwenye mazoezi hayo, Kalson Jeremia (kushoto), George Nkini (katikati) ambae pia ni Naibu waziri wa michezo na burudani SAUTSO.

 

Kocha mkuu wa timu ya soka ya SAUT ambae pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika shahada ya uwalimu akitoa mafunzo kwa vitendo kwenye uwanja wa Raila Odinga.Akizungumza baada ya mazoezi ya timu hiyo kocha mkuu huyo mwenye falsafa ya kuwataka wachezaji wake waingize mazoezi wanayofanya na kuburudika nayo alisema kwamba anaamini timu yake iko vizuri na itafanya vizuri huko iendako.

Wachezaji wakiimba katikati ya mazoezi, falsafa hiyo imekuwa ikipendwa na kocha mkuu wa timu hiyo pale tu wachezaji wanapofanya zoezi gumu huwaamuru waimbe na kucheza pamoja kuwafanya warelax na kufurahia mazoezi.

Mazoezi yakiendelea.

Kwa pamoja kiumakini wakimsikiliza kocha wao katika mazoezi yao Peter Mahenge mwenye track nyeupe.

Ilikuwa ni kwenda na kurudi kwa kasi kubwa kisha unapokea pasi na kurudisha alafu unarudi kwenye mstari wako.

Wanaume kazini. Vijana wakiendelea kulijenga jiji la Mungu.

Vumbi lilikuwa likitimka.

Mwisho walimalizia mazoezi ya viungo na kufunga mazoezi kwa leo, mazoezi hayo yataendelea tena kesho kwenye viwanja vya Raila Odinga chuoni hapo.

One response to “TIMU YA SOKA YA SAUT YAANZA MAZOEZI KUJIANDA NA MECHI ZA KIRAFIKI DHIDI YA BUGANDO NA TOTO AFRICA.

Leave a comment