SAUT YAENDELEA KUJIFUA TAYARI KUWAVAA TOTO AFRICAN ALHAMISI HII CCM KIRUMBA.

  • YAPANIA KUTAFUNA MFUPA ULIOWASHINDA SIMBA.

Timu ya soka ya Chuo cha Mtakatifu Agustino ipo katika mazoezi ya nguvu tayari kuikabili timu ngumu inayosumbua vigogo ligi kuu ya Tanzania bara Toto African ya jijini mwanza katika uwanja wa CCM kirumba  alhamisi ya tarehe 13/10/2011 wiki hii katika mchezo wa kirafiki. Toto African ni timu yenye maskani yake jijini Mwanza na ilitoa upinzani mkali pale ilipocheza na Miamba ya soka Tanzania Bara Simba Sports Club ya Dar es salaam na historia inaonyesha kwamba Toto imekuwa na historia nzuri inapocheza katika uwanja wake huo wa nyumbani. Baada ya mchezo huo dhidi ya Toto African timu hiyo ya SAUT itakuwa na kibarua kingine siku ya Jumamosi itakapoumana na ndugu zao timu ya soka ya chuo kikuu cha tiba cha Bugando mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

SAUT wakiwa katika mazoezi makali katika viwanja vya Raila Odinga chuoni hapo.

 

Kapteni wa timu ya soka ya SAUT ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu shahada ya uongozi wa biashara chuoni hapo baada ya kumaliza mazoezijioni ya leo.

 

Kikosi cha SAUT baada ya Mazoezi yaliyofanyika jioni ya leo Raila Odinga chini ya Kocha mkuu Peter Mahenge.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s