GARI LA KAMPUNI YA NYANZA BOTTLING YA JIJINI MWANZA MANUSURA KUSABABISHA AJALI CHUO CHA MTAKATIFU AGUSTINO-MWANZA

Leo majira ya saa 4:30 Alasirii gari aina ya TATA lenye namba  za usajili T 119 ASQ la kampuni ya vinywaji ya NYANZA BOTTLING  ya jijini Mwanza nusura lisababishe ajali baada ya breki za gari hilo kushindwa kufanya kazi. Kwa mujibu wa Mwanahabari wetu aliyeshuhudia tukio hilo alisema, gari hilo lilizimika na kushindwa kuwaka baada ya kuleta vinywaji katika moja ya canteen chuoni hapo inayojulikana kama SALMACONE, hapo ndipo ilipowalazimu wafanyakazi wa gari hilo kuamuwa kulisukuma ili kuliwasha kwa njia hiyo na mara ya kwanza walipolisukuma breki zake zilikataa kufanya kazi na kujikuta likisimamia kwenye mti uliopo mbele kutokana na spidi kuwa ndogo.

Haikuishia hapo wafanyakazi hao sasa na baadhi ya wafanyakazi wa moja ya canteen ya chuoni hapo walikuja kulisukuma tena gari hilo kwa nyuma na kurudisha kwenye mlima kidogo ili kulifanya lipate spidi ambapo walifanikiwa huku wakitumia kigingi kama breki, baada ya kulisukuma tena kwa mbele dereve wa gari hilo alishindwa kulimudu kutokana na tatizo la breki na kujikuta akiliingiza mtaroni huku akigonga baiskeli ya mwananchi aliyekuwa akisaidia kulisukuma gari hilo. Hii yote ilitokana na uzembe wa dereva wa gari hilo pamoja na wafanyakazi wenzake kutokana na kulijua tatizo la gari hilo lakini wao wakaendelea na kazi hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo.

Wanafunzi na baadhi ya wafanyakazi wakishuhudia ajali hiyo.

Mmiliki wa Baiskeli hiyo akielewzea jinsi baiskeli yake ilivyojeruhiwa huku baadhi ya mashuhuda wakijadiliana kuhusu ajali hiyo ilivyotokea.

Gari aina ya TATA lenye namba T 119 ASQ likiwa kwenye mtaro huku wafanya kazi wa gari hilo wakilikagua baada ya ajali

Gari hilo kwa nyuma baada ya kuingia kwenye mtaro, pembeni kulia ni mti ambao gari hilo lilisimama kwa msaada wa mti huo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s