TAARIFA KWA WAOMBAJI WA MIKOPO.

MAOMBI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA ELIMU YA JUU

KATIKA AWAMU YA PILI (SECOND SELECTION)

KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011/2012

1.0 UTANGULIZI

Kufuatia kutolewa kwa matokeo ya udahili kwa awamu ya pili na Tume ya Vyuo Vikuu, kumekuwepo na wanafunzi wanaofika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo kuulizia juu ya upatikanaji wa mikopo. Kutokana na hali hii, Bodi inapenda kutoa maelezo kwa wanafunzi hao na Umma kwa ujumla juu ya suala hili kama ifuatavyo:

2.0 UTOAJI MIKOPO KWA WANAFUNZI KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011/2012

Bodi ya Mikopo, kwa mwaka wa masomo 2011/2012, imekwishapanga kutoa mikopo kwa wanafunzi 24,628 kati ya wanafunzi 37,924 wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa katika duru ya kwanza (First selection).

Hivyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza na Umma kwa ujumla kuwa bajeti ya ukopeshaji kwa mwaka wa masomo 2011/2012 imekatikia kwa idadi ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo kutoka kwenye kundi la “First selection” ambamo pia takriban wanafunzi 13,296 hawakuweza kupata mikopo. Hivyo, hakuna tena fedha za ukopeshaji kwa wanafunzi wengine.

3.0 HITIMISHO

Waombaji hao wa mikopo na Umma kwa ujumla wanataarifiwa kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu katika duru ya pili au watakaochaguliwa katika duru nyingine zitakazofuatia kuwa hakuna mikopo itakayotolewa kwao kutokana na fedha za ukopeshaji kuishia kwa wale wa duru ya kwanza. Aidha, wakati wa udahili wao, wanafunzi hao wa duru ya pili na duru zilizofuatia, walielezwa bayana na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwamba hawatahusika na mikopo na hivyo udahili wao ni kwa njia ya kujigharamia wenyewe.

Hivyo, wanafunzi husika wanashauriwa kuzingatia maelekezo hayo ya TCU na kuacha kuizonga Bodi kwa kufuatilia mikopo ambayo haitaweza kupatikana kwa mwaka huu wa fedha kutokana na bajeti ya ukopeshaji kuisha.

IMETOLEWA NA:

MKURUGENZI MTENDAJI

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s