SAUT YAITOA JASHO TOTO AFRICAN, YATOKA SULUHU YA BILA KUFUNGANA.

  • KUPAMBANA NA NDUGU ZAO BUGANDO JUMAMOSI KATIKA UWANJA WA NYAMAGANA.

Timu ya soka ya SAUT leo ilikuwa na kibarua kigumu pale ilipokutana uso kwa uso na timu kongwe ya ligi kuu TOTO AFRICAN katika uwanja wa CCM KIRUMBA ambapo timu izo zilitoka suluhu ya bila kufungana. Mchezo kiujumla ulikuwa mzuri kwani pande zote zilishambulia kwa zamu.

Kunako kipindi cha pili timu ya SAUT ilijipatia goli la kwanza lakini mwamuzi wa pambano hilo alilikataa kwa kupiga filimbi ya kusimamisha mpira kwa kisingizio cha mchezaji mmoja alikuwa ameumia ambapo angeweza kupuliza filimbi hiyo kabla ya mshambuliaji huyo kulifikia goli la TOTO. SAUT itakwaana na wapinzani wao wa chuo cha afya BUGANDO katika mchezo mwengine wa kirafiki.

PATA MATUKIO YA MCHEZO HUO KATIKA PICHA.

Mshambuliaji wa TOTO AFRICAN akijaribu kuwatoka wachezaji wa SAUT katika mchezo huo.

Kiungo machachari wa SAUT Kalson Jeremia (mwenye mpira) akikokota mpira na kujaribu kuipita ngome ya TOTO.

Kiungo Kalson Jeremia ambae ni mwanafunzi wa shahada ya Mahusiano ya Jamii na Masoko mwaka wa tatu akimiliki mpira mbele ya kiungo wa TOTO.

Wakati wa mapumziko wachezaji SAUT walikuwa wakipokea mawaidha kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo Peter Mahenge ambae pia ni mwanafunzi wa shahada ya uwalimu mwaka wa pili SAUT huku dokta mkuu wa Timu hiyo Walter Chuwa akitoa huduma kwa Wachezaji.

Wachezaji wa TOTO wakimsikiliza mwalimu mkuu wa timu hiyo John Tegete (katikati).

Mashibiki wakifuatilia mchezo huo kwa makini.

Mashabiki katika mchezo huo.

Wanaume kazini, mabeki wa timu ya SAUT wakijaribu kuokoa hatari gulini kwao.

Mshambuliaji wa TOTO akijaribu kuwatoka mabeki wa SAUT.

Ilikuwa manusura TOTO wapate goli katika kipindi cha pili dakika za mwisho.

Baada ya mpira kwisha mzee Tegete alitaka kumvamia mshabiki mmoja anaesemekana anatoka SAUT kutokana na Maneno makali yaliyomuumiza kocha huo mkuu wa TOTO..

Mashabiki baada ya mpira kumalizika.

Wadau wa VIBE walikuwepo nao kwa aijili ya kuchukua matukio.

Advertisements

2 responses to “SAUT YAITOA JASHO TOTO AFRICAN, YATOKA SULUHU YA BILA KUFUNGANA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s