TAARIFA KUTOKA BODI YA MIKOPO KWA WAOMBAJI WA MIKOPO WAPYA NA WANAOENDELEA.

1.0 FURSA KWA WANAFUNZI WANAOENDELEA NA MASOMO AMBAO HAWAKUJAZA FOMU ZA MAOMBI YA MIKOPO KUJAZA FOMU HIZO

Mchakato wa uchambuzi wa maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2011/2012 umebaini kuwepo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao kwa sababu zisizoeleweka hawakujaza fomu za maombi ya mikopo kupitia njia ya mtandao (OLAS) kama Bodi ilivyokuwa imeelekeza na hivyo kutotengewa mikopo.

Hivyo, Wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao kwa sababu zao hawakujaza fomu za maombi ya mikopo kupitia mtandao (OLAS) wanapewa fursa ya mwisho ya kuonyesha uhitaji wao wa mikopo. Hivyo, wanafunzi hao wanatakiwa kujaza fomu za maombi ya mikopo kupitia mtandao kwa anuani: olas.heslb.go.tz. Maombi yote yafanyike katika kipindi kisichozidi wiki mbili kuanzia tarehe 12 Oktoba, 2011. Hakutakuwa na muda wa ziada baada ya muda huo kuisha.

Aidha, Bodi inapenda kuwatahadharisha wanafunzi husika kuwa kutokana kushindwa kwao kuomba mikopo kwa wakati, kutakuwa na uchelewesho wa mikopo hiyo. Hivyo, itabidi wawe na subira wakati mchakato wa kuandaa mikopo hiyo ukifanyika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za utoaji mikopo.

Orodha kamili ya wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawakujaza fomu za moambi ya mikopo inapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo: www.heslb.go.tz.

2.0 FURSA KWA WAOMBAJI WAPYA WA MIKOPO KUREKEBISHA FOMU ZAO ZA MAOMBI YA MIKOPO AMBAZO ZINA DOSARI.

Uchambuzi wa maombi ya mikopo kwa waombaji wapya umebaini kuwa waombaji wa mwaka wa kwanza wapatao 1,115 waliodahiliwa katika programu za ualimu wa sayansi, ualimu wa hesabu na sayansi za tiba hawajapata mikopo kutokana na kutosainiwa kwa fomu za maombi/ mikataba au kutoambatanisha vyeti vya kuzaliwa.

Hivyo, wanafunzi hawa pia wanapewa fursa ya kurekebisha mapungufu hayo ndani ya kipindi cha wiki mbili kuanzia tarehe 12 Oktoba, 2011 ili waweze kukidhi vigezo vya kutengewa mikopo. Kwa hiyo, wanafunzi hao watalazimika kufika kwenye Ofisi za Bodi ya Mikopo ili kurekebisha mapungufu hayo, kwa gharama zao wenyewe. Aidha, wanafunzi hawa wanataarifiwa kuwa kutakuwa na uchelewesho wa mikopo kwa sababu ya dosari zilizojitokeza na hivyo wanatakiwa kuwa na subira wakati mchakato wa kuandaa mikopo hiyo ukiendelea.

Orodha kamili ya wanafunzi hao ambao fomu zao za maombi ya mikopo zina dosari inapatikana kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo: www.heslb.go.tz.

3.0 HITIMISHO

Waombaji wote wanahimizwa kutekeleza maelekezo haya ndani ya kipindi cha wiki mbili kama ilivyoelekezwa. Baada ya muda huo kuisha hakutakuwa na muda wa ziada na hivyo watakaoshindwa kutekeleza hawataweza kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2011/2012. Aidha, ni wanafunzi hao tu walio kwenye orodha hizo mbili ndio wanaohusika na tangazo hili, siyo mwingine yeyote.

IMETOLEWA NA:

MKURUGENZI MTENDAJI

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s