WANAFUNZI TEOFILO KISANJI (TEKU) JIJINI MBEYA WAANDAMANA KUTOKANA NA KUCHELEWA KWA MIKOPO YAO.

Wanafunzi wapatao 4500 wa chuo kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini mbeya wameandamana mpaka kwa mkuu wa mkoa wa mbeya kwa mdai ya kucheleweshewa pesa zao za mikopo kuotoka bodi ya mikopo. Wanafunzi hao mabao maandamano yao yaliyozuiliwa na polisi wa kutuliza ghasia jijini mbeya yalianzia chuoni hapo mpaka kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa mbeya.

Rais wa wanafunzi wa chuo hicho ndugu Ambukege Imani alisema kuwa waliwasilisha maombi ya kibali cha maandamano hayo ya amani kwa jeshi la polisi lakini jeshi hilo lilikataa kuwapatia kibali hicho. Rais alidai kwamba wanafunzi wa chuo hicho walifadhaishwa na taarifa zilizotolewa na bodi ya mikopo kwamba pesa zao zitatolewa mwezi Disemba huku wanafunzi katika vyuo vingine wakiwa tayari wameshapewa pesa zao.

 Akizungumzia suala hilo, Waziri wa mikopo chuoni hapo alisema kwamba wanafunzi wanaishi katika hali ngumu hali inayowafanya washindwe kuzingatia masomo na kutokana na majibu ya bodi kutoridhisha ndio sababu ya wanafunzi hao kuchukua hatua hiyo ya kuandamana kama njia ya kuelezea madai yao baada ya kutoona matumaini.

Wanafunzi wakiwasikiliza viongozi wao (Hawapo pichani)

Wanafunzi hao wakielekea katika ofisi za mkuu wa mkoa.

Magari ya polisi yakiwa tayari kuzui maandamano hayo.

 

Rais wanafunzi chuoni hapo (Mwenye Suti) na Waziri mkuu wake wakizuiliwa kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wakirudishwa walikotoka na askari wa kutuliza ghasia mkoani mbeya.

Wengine waliandika ujumbe wao kwenye mabango ili mradi ujumbe uweze kuwafikia wahusika. Natumai ujumbe umefika.

 CHANZO CHA HABARI.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s