SAUT YAFANYA MADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KWA MDAHALO.

MADA: Miaka hamsini ya uhuru na Maadui Watatu wa Mwalimu Nyerere.

REV. DK. KITIMA: Elimu ndio itakayotukumboa katika matatizo yote sugu ya nchi hii.

DK. SAFARI: Utajiri unaleta Umasikini.

NKWABI: Nyerere Alikuwa na Kipaji, Hekima na Uwadilifu sifa zinazomtofautisha na viongozi 

                     wengine Afrika.

Serikali ya wanafunzi ya Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza jana kilifanya mdahalo wa pamoja katika kuadhimisha miaka 12 tangu kifo cha hayati Baba wa Taifa hili Mwl. Julius Kambarage Nyerere kufariki tarehe 14/10/1999. Katika Mdahalo huo Mada kuu ilikuwa  ni  Miaka hamsini ya uhuru na Maadui Watatu wa Mwalimu Nyerere. Wageni waalikwa walikuwa ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Rev. Dr. Charles Kitima ambae alizungumzia Elimu na Falsafa ya Mwalimu kiujumla, Dk. Safari Isaac ambae alizungumzia Umaskini,  Nkwabi Ng’wanakilala ambae alizungumzia Afya katika falsafa ya Mwalimu.

 Mdahalo ulianza baada ya Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza Mh. Cosmas Mataba kufungua Rasmi kwa kumkaribisha Makamu mkuu wa chuo. Mdahalo huo amabao ulikuwa na wahudhuriaji wachache kutokana na hali ya hewa iliyokuwepo asubuhi ya jana jijini mwanza ambapo mvua kubwa ilinyesha hivyo kuwafanay wanafunzi wengi wasipate nafasi ya kuhudhuria mdahalo huo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dk. Kitima alizungumzia Elimu na jinsi gani mwalimu alivyosimamia Elimu kwa kuwasomesha wasomi wa nchi hii ambapo bila ya falsafa ya Mwalimu yeye asingeweza kufika hapo alipofika. Alisema elimu ndio itakayotukomboa katika matatizo yetu sugu katika nchi hii na kama ikitumika vizuri matatizo hayo sugu yanaweza kuisha kwa muda mfupi na maadaui watatu wa Mwalimu wataisha kwa kutumia elimu. Aliongeza kwa kusema kama wanafunzi hawatokuwa na uzalendo na nchi hii kama Nyerere hawatakuwa Viongozi wazuri wa nchi hii hapo baadae. Mfumo wa Nyerere uliandaa watu wa kuweza kufanikisha falsafa yake inafanikiwa katika nchi hii hivyo aliwaasa wanafunzi kuweza kuona na kuenzi maono ya Mwalimu kwani kosa linalofanywa ni kusahau kuiga na kuendeleza hatua ya pili ya falsafa ya Mwalimu Nyerere. Mwisho alisema kuwa Tanzania inahitaji uhuru wa kiuchumi inaoumiliki wenyewe ivyo haina budi kuanda wasomi watakao weza kuendeleza uchumi wa nchi hii.

Dr. Kitima kutoka wa pili kutoka kulia, Nkwabi Ng'wanakilala wa kwanza kulia, na Rais wa Setikali ya Wanafunzi (kushoto) wakisikiliza kwa makini mada kuhusu umaskini kutoka kwa Dk. Safari hayuko pichani.

 

Dk. Safari Isaac ambae ni Director wa Rev. Mgulunde Learning Resources Centre ambayo ndio Library ya Chuo hicho akitoa mada juu ya Umasikini. Mazungumzo yake yalijikita kuelezea Umaskini na jinsi gani falsafa za Mwalimu zilitumika juu ya umasikini. Katika maongezi yake yaliyozama kwenye Theories juu ya umasikini Dk. Sfari aliacha swali miongoni mwa Washiriki pale aliposema kuwa Utajiri unaleta Umasikini Nchini, Pia aliweza kutumia misema kutoka kwa watu mbalimbali mabapo alimnukuu Mahtama Gandhi "Mtu mwenye njaa ataendelea kuongelea malalamiko zaidi ya umasikini kuliko kuongelea maendeleo" Umasikini unawafanya watu wawe watumwa kwa kupunguza uwezo wa kufikiri.

 

Nkwabi Ng'wanakilala Senior Lecture SAUT akitoa mada juu ya Afya, Ni mmoja kati ya watu waliofanya kazi kwa pamoja na Mwalimu na alimuelezea Mwalimu kama mtu mwenye Kipaji, Hekima na Uwadilifu sifa mbazo zinamfanya Mwalimu awe mtu wa kipekee katika viongozi wa bara hili la Afrika. Maadui watatu wa mwalimu sasa wanatumika kama misingi mikuu ya rushwa na matatizo ya nchi, Afya inaweza ikakufanya kuweza kunyimwa haki yako na ndio Mwalimu alikuwa amelisimamia ili kuondoa unyonyaji wa wananchi. Swala la Afya lilikuwa ni swala muhimu akatoa mfano Mwaka 1975 kulikuwa na kampeni za "Mtu ni Afya" ambayo lengo lake lilikuwa ni kumshirikisha kila mtu kwenye kila kijiji, kutokana na maadili na heshima pamoja na wito wa Mwalimu Nyerere ndani ya wiki moja watu milioni tatu waliweza kushiriki kwenye kampeni hizo nchi zima na kwa wakati huo kulikuwa na watu takribani milioni kumi na mbili.

 

Rais wa Serikali ya wanafunzi SAUT Mh. Cosmas Mataba akielezea mchango wa mwalimu katika kuiendeleza nchi hii.

 

Alfred Fanuel mwanafunzi wa mwaka watatu Ualimu akitoa mawazo yake katika mdahalo huo, alisema kuwa Watanzania wanatakiwa kuazimisha siku ya kifo cha Mwalimu Nyerere kwa kuyafanyia kazi yale aliyoyaanzisha na kuyaacha.

 

Mwenyekiti wa CCM tawi la SAUT Mh. Yaredi nae alikuwa akitoa mchango wake ambapo alisema kuwa wasomi wa nci hii hawana uzalendo na nchi yao kwani wengi wao wamekuwa wakikimbilia nje yanchi kufanya kazi badala ya kujenga nchi yao na ili kukabiliana na umasikini ni lazma wanachi wote kwa pamoja na viongozi wa nchi hii tuungane ili kupambana na changamoto zilizopo.

 

Ester Karugendo Mwanafunzi wa mwaka wa pili uwalimu akichangia mada kwa kusema kuwa uongozi mbovu ndio chanzo cha matatizo yote yanayoikabili nchi hii.

 

Mgeni kutoka Africa Youth Leadership Forum, Peter Nyalandu nae alikuwepo katika kuchangia maoni yake katika mada ya mdahalo huo, alisema kuwa tatizo la nchi hii ni viongozi kutofata misingi ya Mwalimu katika maadili ya majukumu waliyonayo.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s