SAUT YAWAONEA NDUGU ZAO BUGANDO. YAWAFUMUA MAGOLI MATATU BILA YA MAJIBU.

Timu ya soka ya SAUT jumamosi ya mwisho wa wiki hii iliwashushia kipigo ndugu zao wa chuo cha afya Bugando kwa kuwafunga goli tatu bila ya majibu. Mchezo huo amabo ulikuwa ni wakusheherekea na kuipongeza Bugando kwa kupanda hadhi na kuwa chuo kikuu kamili. Mcheoz huo uliochezwa kwenye uwanja wa wilaya ya Nyamagana(Nyamagana Stadium) ulihudhuriwa na mashabiki wengi wa Bugando kuliko SAUT. Mchezo huo ulioshuhudiwa na Maaskofu ulianza kwa kasi na SAUT walijipatia magoli mawili kipindi cha kwanza ambapo goli la kwanza lilifungwa na mshambuliaji Iddi Mande (Motiso) kabla ya Domy kufunga goli la pili na timu kwenda mapumziko. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kila timu kushambulia kwa zamu alikuwa Motiso tena aliyewanyanyua mashabiki wachache wa SAUT kwa kufunga goli la pili.

PATA MATUKIO KATIKA PICHA.

Askofu na Makamu Mkuu wa chuo cha Bugando mwenye Suti nyeusi wakimsindikiza askofu mkuu wa jimbo la Iringa akienda kupiga penati kuashiria kufungua mchezo huo.

Askofu Mkuu wa jimbo la Iringa akijianda kupiga penati ambapo alifunga goli safi kabisa baada ya kumpeleka kipa kulia na mpira kwenda kushoto.

 

Askofu wa Jimbo la Iringa Tarcsius Ngalalekumtwa (Mwenye Miwani) akiwa tayari kushuhudia mchezo huo.

 

Hatari katika lango la Bugando.

 

Hatari katika lango la SAUT.

 

Wachezaji wa SAUT wakimpongeza mshambuliaji wao Motiso baada ya kufunga goli la kwanza huku mabeki wa Bugando wenye nyeupe wakilaumiana.

 

Mshambuliaji Domy (kulia) akishangilia goli la pili kwa timu yake baada ya kufunga goli hilo.

Ni Motiso tena akipongezwa baada ya kufunga goli la pili.

Kocha wa Timu ya SAUT akitoa mawaidha kwa timu yake wakati wa mapumziko.

Kocha wa Bugando akitoa maelekezo kwa timu yake wakati wa mapumziko.

 

Mwisho wa siku SAUT 3-0 BUGANDO.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s