WANAFUNZI CHUO CHA MKWAWA (MUCE) IRINGA WAANDAMANA HADI NMB.

Kuotoka kwa Francis Godwin Blog, Iringa.

WANAFUNZI zaidi ya 100 wa mwaka wa tatu na wa pili katika chuo cha elimu Mkwawa (MUCE) leo wameaandamana hadi benki ya NMB tawi la Mkwawa mjini Iringa kushinikiza uongozi wa benki hiyo kuwaingizia fedha zao kutoka bodi ya mikopo katika akaunti zao.

Wanafunzi hao walifanya maandamano hayo ya amani jana majira ya asubuhi na kupiga kambi ya muda nje ya viwanja vya benki hiyo ya NMB tawi la Mkwawa iliyopo eneo la kata ya Gangilonga mjini Iringa huku wakiutaka uongozi wa benki hiyo kutekeleza madai yao ya kuingiziwa fedha zao katika akaunti zao baada ya bodi ya mikopo kuwata taarifa juu ya kutumiwa fedha zao hizo.

Wakizungumza na mtandao huu wanafunzi hao walisema wameshindwa mkuvumilia kitendo cha kucheleweshewa kuingiziwa fedha zao katika akaunti na hivyo kulazimika kufika kukutana na uongozi wa benki hiyo ili kujua sababu ni nini baada ya wenzao katika vyuo vingine kuingiziwa fedha hizo.

Hata hivyo walisema benki ya CRDB inaonyesha hundi ya wanafunzi ambao ni wateja wa NMB ilipelekwa katika benki hiyo kwa zaidi ya siku mbili ila baada ya wao kwenda kutazama salio katika akaunti zao hawakuweza kuona jipya.

Wanafunzi hao walisema kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 650000 wanazodai kiasi cha shilingi 450,000 ni fedha kwa ajili ya chakula na malazi na kiasi cha shilingi 200,000 ni fedha za stationary .
Waziri wa mikopo katika chuo cha Mkwawa Kikumbi Mohamed alipongeza majibu mazuri yenye ufafanuzi yaliyotolewa na uongozi wa benki hiyo na kuwa bado tatizo la ucheleweshaji wa fedha hizo halijajulikana.

Hata hivyo alisema kuwa katika suala hilo na mgomo kufanya maandamano ya amani wao wanaipongeza serikali kwa kutimiza madai yao ya kuwapa fedha hizo ila kama kuna mapungufu ni ya kiutendaji yaliyotokana na chuo ama benki hiyo.

Katika mgomo huo uliodumu kwa zaidi ya masaa mawili kwa wanafunzi hao kukusanyika nje ya mlango wa benki hiyo ,uongozi wa benki hiyo uliweza kukutana na wawakilishi wa wanafunzi hao na kuwataka wanafunzi hao kuvuta subira wakati wakiendelea kuchelewesha .

Matukio Zaidi Katika Picha.

Mmoja kati ya viongozi wa wanafunzi akitoa ufafanuzi aliopata kwa uongozi wa benki ya NMB.

Wanafunzi chuo cha Mkwawa wakipinga uamuzi wa kuingiziwa fedha zao kesho.

Wanafunzi chuo cha Mkwawa Iringa wakiwa wamepiga kambi nje ya benki ya NMB Iringa kushinikiza kuingiziwa fedha zao za mikopo.

Nje ya Benki ya NMB.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s