REDD’S ORIGINAL WAJA NA TAMASHA LA MITINDO LIJULIKANALO KAMA ”REDD’S UNI-FASHION BASH” KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NCHINI.

TAZAMA HABARI YA UZINDUZI HUO.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imezindua shindano la aina yake la mitindo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kupitia kinywaji chake cha REDD’S ORIGINAL. Shindano hilo litakalojulikana kama ”REDD’S UNI-FASHION BASH” litaanza mwezi huu wa Octoba mpaka Novemba mwaka huu na kushirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu vilivyo kwenye mikoa minne ya Dar es salaam, Kilimanjaro, Dodoma na Mwanza.

Akizungumza katika uzinduzi wa shindano hilo Meneja wa Kinywaji cha REDD’S ORIGINAL Bi. Victoria Kimaro alisema “Tamasha hili la mitindo lina lengo la kuinua vipaji vya wanafunzi wa elimu ya juu kwenye tasnia hii ya mitindokupitia maonesho yatakayofanywa katika vyuo, ambapo wanafunzi wenye vipaji vya ubunifu watapata fursa ya kuonesha vipaji vyao vya ubunifu wa mitindo. Hii ni fursa kubwa kwao kujitangaza na kudhihirisha vipaji vyao.

Bi Kimaro pia alieleza utaratibu wote wa kuwapata wabunifu watakaoonesha kazi zao jukwaani wakati wa tamasha hili. Alisema kuwa “Uzinduzi huu utafuatiwa na usajili wa wanafunzi wabunifu na wanamitindo kupitia fomu maalum zitakazosambazwa vyuoni kisha majaji watachambua fomu zote zitakazowasilishwa na kupata washindi kumi kutoka kila mkoa watakaokidhi vigezo, ambao watapata fursa ya kuonesha mavazi yao jukwaani, pia kutakuwa na nafasi kumi kwa wanamitindo watakaovaa mavazi hayo jukwaani.

Majaji watakaa na kuangalia washindi na kupata zawadi kutoka kinywaji cha Redd’s Original.

Akizungumzia zawadi za washindi meneja wa masoko wa TBL Fimbo Butallah alisema “Zaidi ya kuwapatia jukwaa wabunifu na wanamitindo hao ili kuonesha vipaji vyao, Redd’s pia itawapatia zawadi za washindi watano kutoka kila mkoa watakaoshika nafasi za juu kama ifuatavyo.

WABUNIFU

MSHINDI WA KWANZA 700,000

MSHINDI WA PILI 500,000

MSHINDI WA TATU 300,000

NSHINDI WANNE NA WATANO 100,000 KILA MMOJA.

WANAMITINDO

MSHINDI WA KWANZA 500,000

MSHINDI WA PILI 400,000

MSHINDI WA TATU 300,000

NSHINDI WANNE NA WATANO 100,000 KILA MMOJA.

Tunaimani kubwa zawadi hizi zitaongeza chachu kwa wabunifu kujidhatiti katika kuendeleza ubunifu katika tasnia hii ya mitindo. Lakini pia matamasha haya yatashirikisha burudani mbalimbali za kuvutia hivyo kufanya sehemu muhimu ya kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo na kada malimabali katika kufurahia na kubadilishana mawazo katika maswala ya mitindo.

Kinywaji cha Redd’s kimekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza tasnia ya urembo, ubunifu na mitindo hapa nchini.

Meneja Masoko TBL Fimbo Butallah akitoa ufafanuzi juu ya Shindano hilo la ubunifu kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka vyuo vya mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Dodoma na Mwanza.

Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original Bi. Victoria Kimaro akionesha fomu itakayotumiaka na washiriki kujiunga na shindano hilo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa TBL, Edith Mushi na Kushoto ni Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah.

CHANZO CHA HABARI.

Advertisements

2 responses to “REDD’S ORIGINAL WAJA NA TAMASHA LA MITINDO LIJULIKANALO KAMA ”REDD’S UNI-FASHION BASH” KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NCHINI.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s