WANAFUNZI 191TU ZANZIBAR KATI YA 1603 KUPATA MIKOPO.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ramadhan Abdalla Shaaban akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu swala la baadhi ya wanafunzi zanzibar kukosa mikopo kutokana na sababu mbalimbali.

Na Fatma Mzee-Maelezo Zanzibar

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar imesema kuwa wanafunzi walioomba masomo ya Shahada ya Sheria, Utawala wa Umma, Ualimu wa Lugha ya Kiarabu na Dini ya Kiislamu hawatapatiwa mkopo kwa sababu tayari wahitimu wa fani hizo wako wengi katika soko la ajira.

Aidha wasomi wa taaluma hizo wapo wengi katika vyuo vya elimu ya juu jambo ambalo linasababisha kutopewa kipaumbele fani hizo katika mikopo.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ramadhan Abdalla Shaaban ameyasema hayo ofisini kwake alipokuwa akitoa taarifa juu ya wanafunzi watakaopatiwa udhamini wa masomo ya juu kwa kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Zanzibar kwa mwaka 2011/2012

Amesema kwa mwaka huu idadi ya wanafunzi watakaopatiwa mikopo ni 191tu, kati ya wanafunzi 1603 walioomba kupatiwa mkopo na Bodi hiyo.

Miongoni mwa wanafunzi hao 1603 walioomba kupatiwa mkopo na Bodi hiyo ya Zanzibar wanafunzi 1025 wameomba kwa ajili ya kujiunga na vyuo vya ndani ambapo kwa upande wa vyuo vya nje walioomba ni wanafunzi 2011.

Waziri Shaaban amesema idadi ya wanafunzi 1603 ni kubwa ikilinganishwa na mwaka jana ambapo maombi ya wanafunzi 1025 yalipokelewa, hali inayoonyesha ongezeko la wanafunzi wenye sifa za kujiunga na Elimu ya Juu kwa asilimia 60 mwaka huu.

Aidha wanafunzi wanaojiendeleza kwa Post Graduate Diploma, Shahada ya Pili na Shahada ya Tatu nao pia hawatapatiwa mkopo ili kutoa nafasi kwa vijana wengi wa shahada ya kwanza wenye sifa nzuri za kujiunga na vyuo.

Majina ya wanafunzi hao watakaopatiwa Mkopo na Bodi hiyo ya Zanzibar yatachapishwa katika Gazeti la Zanzibar Leo na majina yao pia yatawekwa katika tovuti ya Wizara ya Elimu

Wakati huo Waziri Shaaban ametoa wito kwa wazazi wa wanafunzi ambao hawakupata mikopo kujitahidi kuwasomesha watoto wao kwa gharama zao kwani kufanya hivyo ni kuwekeza.

Jumla ya shl. Bilion 7.8 zimekopeshwa kwa wanafunzi mbali mbali na wengine tayari wameshamaliza masomo yao na kuajiriwa hivyo wanapaswa kurejesha fedha hizo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s