WANAFUNZI UDOM KUSAJILIWA KWA KIAPO,WAANZA USAJILI LEO UWANJA WA JAMHURI.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wa Mwaka wa pili na wa tatu jana wameanza usajili mpya wenye kanuni katika kile kinachoonekana kuzuia tabia za migomo kwa wanafunzi wa chuo hicho. Usajili huo unaofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma ulianza kufanyika kuanzia majira ya saa 8.00 asubuhi katika viwanja hivyo.

Tangazo la chuo hicho lililotolewa na Uwongozi wachuo linawataka wanafunzi wote wanaodaiwa kutakiwa kulipa kwanza madai yao kabla ya kufanya usajili, pia kila mwanafunzi anatakiwa kulipa gharama za usajili kiasi cha shilingi 10,000/=, Kila mwanafunzi ni lazima akaape kwa wakili kiapo cha utii wa sheria ndogondogo za wanafunzi za chuo kikuu cha Dodoma, sheria za chuo kikuu cha Dodoma na za nchi. Ambapo Kiapo kinatakiwa kubandikwa picha Mbili (2) za ‘passport size’ ; Moja ya mzazi/mlezi na moja ya mwanafunzi muhusika.. Katika taarifa hiyo inasema kuwa “Mwanafunzi atakaekiuka kiapo chake atafukuzwa chuo mara moja”

Kila mwanafunzi pia anatakiwa kwenda na nakala halisi za vithibitisho vya malipo yote ya ada na gharama nyingine kuanzia alipoanza masomo, pia ni lazima aende na kithibitisho cha kiapo cha utii.Mwanafunzi ambae hatatimiza masharti hayo hataweza kupokelewa Chuoni.

Usajili huo unaoenda katika makundi kama ifuatavyo:

“Thursday 20th October 2011, Second year Students in the
College of Humanities and Social Sciences; Friday 21st October 2011, Second year Students in the
Colleges of Informatics and Virtual Education, Natural and Mathematical Sciences, Earth Sciences, Education and Health
Sciences; Saturday 22rd October, Third year Students in College of Humanities and Social Sciences; Sunday 23rd October 2011, Third year Students in the Colleges of Informatics and Virtual Education, Natural and Mathematical”.

Plosis nao walikuwepo katika kuangalia usalama kwenye zoezi hilo katika uwanja wa jamhuri Dodoma.

Wanafunzi wakiwa katika harakati za kuchukua namba kabla ya kuingia ndani ya uwanja huo.

Wanafunzi hao wakiwa katika foleni ya kwenda kufanya usajili huo.

Advertisements

One response to “WANAFUNZI UDOM KUSAJILIWA KWA KIAPO,WAANZA USAJILI LEO UWANJA WA JAMHURI.

  1. ni mchakato mzuri.lakini swali langu ni kwamba kwa kusaini huko hicho kiapo hata kama haki zako umenyimwa huwezi kudai.huku tunarudi kule kule kwenye bougus treaties.sijui tanzania tunajenga taifa la namna gani.huu ni udicteta.I STRONGLY DISAGREE WITH THIS.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s