AIESEC-SAUT WAPEWA SEMINA YA UZAZI NA UKIMWI TOKA UMATI.

 AIESEC, chama cha vijana kinachojishughulisha na ugunduzi na ukuzaji wa kipaji cha Kijana kwenye maswala ya uongozi ili kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii leo kimepewa semina juu ya maswala ya elimu ya uzazi na maambukizi ya UKIMWI kutoka kwa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI). Semina hiyo imefanyika katika vikao vya tawi hilo la AIESEC SAUT ambapo vijana zaidi ya thelathini ambao ni wanachama wa chama hicho waliweza kupata elimu hiyo ya afya ya uzazi.

Akizungumza katika semina hiyo Mratibu wa Vijana UMATI, Bi Jacinta K.Mutakyawa alisema kuwa jamii inatakiwa ijue haki ya kila mtu na kuhakikisha haki hiyo inaheshimiwa na kulindwa. Bi Jacinta alisema kuwa swala la Afya ya Uzazi ni jambo muhimu amabalo vijana wanatakiwa kupewa elimu yake kwani matokeo yanayojiri kwenye jamii ni kwa sababu vijana wengi na hata walio vyuo vikuu hawana elimu kabisa au elimu ya kutosha juu ya afya ya uzazi kutokana na jamii kutolichukulia kwa mkazo swala zima la afya ya uzazi na ujinsia.

Bi. Jacinta alielezea juu ya Azimio la International Planned Parenthood Federation (IPPF ) juu ya Haki za Afya ya Uzazi na Ujinsia, alisema kuwa” Azimio la IPPF kuhusu haki za afyaya uzazi na ujinsia ni mwongozo wa kimaadili ambao IPPF inautumia kutekeleza majukumu yake.Haki za afya ya uzazi na ujinsia ni haki na uhuru wa watu binafsi na wanandoa ambazo zimejengwa katika misingi ya sheria za kimataifa za haki za binadamu”.

Haki hizo ni Haki ya Kuishi, Haki ya Uhuru na Usalama wa Mtu, Haki ya Usawa na Kuwa Huru Kutokana na Aina Zote za Ubaguzi, Haki ya Faragha, Haki ya Uhuru wa Fikra, Haki ya Kupata Habari na Elimu, Haki ya Kuchagua Kuoa/Kuolewa na Kutooa/Kutoolewa na kuanzisha Familia, Haki ya Kuamua kupata /Kutopata Watoto na Lini Kuwapata Watoto hao, Haki ya Huduma za afya na kinga, Haki ya Kunufaika na Maendeleo ya Kisayansi, Haki ya Uhuru wa Kukutana na Kushiriki Katika Siasa, pamoja na Haki ya Kutoteswa na Kutendewa Vibaya. Ambapo kama Haki hizo zinazingatiwa na jamii basi matatizo yanayotokana na Afya za uzazi na Ujinsia zitaweza kupungua kama si kutoweka kabisa.

Bi. Jacinta K.Mutakyawa , Mratibu wa Vijana kutoak UMATI akitoa elimu Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Wanachama wa AIESEC-SAUT.

Bi. Jacinta akitoa mawaidha yake huku wanachama wa AIESEC-SAUT wakimsikiliza kwa makini.

Mwakilishi kutoka (YAM) Harakati zza Vijana kwa Vitendo Tanzania, Bw. Petro Itovya, akitambulisha chama hicho cha vijana kilicho chini ya UMATI ambacho kazi yake kubwa ni kukutanisha viajan kwa pamoja katika ktuoa sauti zao na kujitoa kuwa wanaharakati kwa vitendo wakielimisha vijana na kuhamasisha mabadiliko chanay juu ya elimu ya afya ya uzazi na ujinsia Tanzania. Ambapo alizungumzia juu ya upataji wa wanachama wa chama hicho na kuwataka vijana wa AOESEC kujiunga na chama hicho.

AIESEC-SAUT pamoja na wana-UMATI wakicheza Rollcall baada ya semina hiyo kwisha.

Rolcall kutoka kwa member wa AIESEC-SAUT

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s