WANAFUNZI UDOM WAJIKUTA KATIKA HALI TATA JUU YA HATMA YAO YA MIKOPO.

Wanafunzi wapatao 1087 wa chuo kikuu cha Dodoma wamejikuta katika wakati mgumu juu ya hatma ya mikopo yao baada ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kutoa orodha ya majina ya wanafunzi ambao hawakujisajili kwa ajili ya kuomba mikopo kwa mwaka mpya wa masomo katika mfumo mpya wa mtandaoni kwa waombaji wa mikopo (OLAS).

Kwa mujibu ya Taarifa ya Bodi ya Mikopo iliyotoka Alhamisi ya tarehe 13/10/2011 inasema

“Mchakato wa uchambuzi wa maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2011/2012 umebaini kuwepo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao kwa sababu zisizoeleweka hawakujaza fomu za maombi ya mikopo kupitia njia ya mtandao (OLAS) kama Bodi ilivyokuwa imeelekeza na hivyo kutotengewa mikopo.

Hivyo, Wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao kwa sababu zao hawakujaza fomu za maombi ya mikopo kupitia mtandao (OLAS) wanapewa fursa ya mwisho ya kuonyesha uhitaji wao wa mikopo. Hivyo, wanafunzi hao wanatakiwa kujaza fomu za maombi ya mikopo kupitia mtandao kwa anuani: http://olas.heslb.go.tz. Maombi yote yafanyike katika kipindi kisichozidi wiki mbili kuanzia tarehe 12 Oktoba, 2011. Hakutakuwa na muda wa ziada baada ya muda huo kuisha.

Aidha, Bodi inapenda kuwatahadharisha wanafunzi husika kuwa kutokana kushindwa kwao kuomba mikopo kwa wakati, kutakuwa na uchelewesho wa mikopo hiyo. Hivyo, itabidi wawe na subira wakati mchakato wa kuandaa mikopo hiyo ukifanyika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za utoaji mikopo”.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiwa katika mchakato wa kuhakikisha hawakosi boom mwaka huu wakati walipokuwa wakijaza fomu za bodi za kuombea mikopokwa njia ya mtandao kwa wanafunzi wanaondelea mwaka wa pili na wa tatu. Leo ndio mwisho wa kufanya usajili huo kwa wasiojaza fomu hizo kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Mikopo. Picha zote ni kwa Hisani ya Blog ya Matukio na Wanvyuo


Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s