KUTOKA UDOM: WANAFUNZI 551 WALIOFUKUZWA HAWAJAREJEA CHUONI.

Wanafunzi 551 waliokuwa wamefukuzwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), hawajarejea chuoni tangu chuo hicho kilipofunguliwa wiki moja iliyopita. Wanafunzi hao wanaendelea kuhojiwa na Kamati ya Maadili na mpaka sasa ni 55 tu waliohojiwa. Mbali na hao, wengine 126 wako hatarini kufukuzwa baada ya kusaini wenyewe barua ya kutorudi chuoni wakitaka wenzao watatu waliosimamishwa warejeshwe kwanza.  Akizungumza na gazeti la HabariLeo juzi, Ofisa Uhusiano wa Chuo hicho, Beatrice Baltazary, alisema kati ya walio hatarini kufukuzwa, 41 ni wa Shahada ya Sayansi katika Hisabati na 85 wa Shahada ya Sayansi katika Takwimu.

Alisema wanafunzi hao walisaini barua za kutorejea chuoni mpaka wenzao waliokuwa wakiwatetea wanaosubiri kuhojiwa na Kamati warejeshwe.

Alifafanua, kuwa iwapo wanafunzi wanaohojiwa watabainika kuwa na hatia basi hao 126 watakuwa wamejifukuzisha chuo; lakini wasipokutwa na hatia nao watarejea chuoni.  “Walikuwa wakidai kurejeshwa kwa wenzao waliokuwa wamesimamishwa masomo na kusaini sehemu mbili tofauti, kudai kama wenzao hawatarejeshwa chuoni na wao hawataki kurejea, hivyo kurejea kwao kunategemea uamuzi wa hawa watatu,” alisema.

Akizungumzia wanaoendelea kuhojiwa, alisema ni kutoka vitengo vya Kompyuta na Mawasiliano, Sayansi ya Jamii na Shahada ya Sayansi katika Hisabati . Alisema baada ya kumaliza kuwahoji, uamuzi utatolewa kuhusu watakaorejeshwa chuoni na watakaotakiwa kujieleza, huku akisisitiza kuwa hakuna jinsi ya wanafunzi hao kuchelewa masomo, kwani lazima matatizo hayo yatatuliwe kwa kufuata taratibu.  “Siwezi kusema kuwa wanafunzi hawa watarudia mwaka, kwani wenzao ndio wana wiki moja tangu warejee, hivyo baada ya kumaliza kuwahoji, Kamati itatoa majibu na taratibu zingine zitafuata,” alisisitiza Baltazary.

Alisema kwa wanafunzi wa Chuo cha Kompyuta, Habari na Mawasiliano, watamaliza kuhojiwa mwishoni mwa wiki hii na matokeo kutolewa. Wanafunzi wa chuo hicho, walilalamika kuwa baadhi yao bado hawajarejeshwa chuoni tangu wasimamishwe, huku kukiwa na tetesi za kurudia mwaka kwa wasiorejeshwa.

Wanafunzi hao wa Chuo cha Sanaa na Sayansi za Jamii, walisimamishwa masomo Juni 14, baada ya kugoma na kuandamana kwa madai mbalimbali. Jumla ya wanafunzi 9,000 walifukuzwa kwa madai ya kuhamasisha mgomo usio halali na kwamba uongozi wa chuo uliwataka kuondoka kabla ya saa 8 mchana siku hiyo.

CHANZO CHA HABARI.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s