UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA WATISHIA MAISHA YA WANAFUNZI WAISHIO HOSTEL ZA NJE SAUT MWANZA

Matukio ya unyang’anyi yamekuwa yakitokea maeneo ya Chuo cha Mtakatifu Agustino ambapo baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakinyang’anywa vitu vyao vya thamani na hata kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali.

Siku ya Jumatatu tarehe 24/10/2011 majira ya saa nne za usiku mabinti watatu walivamiwa maeneo ya karibu na hosteli za chuo hicho za Rugambwa, ambapo kati yao wawili waliojulikana kwa jina moja moja ni Getrude na Neema,wanafunzi wa shahada ya masomo ya jamii mwaka wa 3 (BA. in Sociology) na tukio lingine ni la mwanafunzi wa shahada ya mawasiliano ya umma mwaka wa 3 (BA. in Mass Communication) Jaysam Jeremiah  lililotokea tarehe 25/10/2011 majira ya saa 5:30 usiku siku moja baada ya kutokea tukio la kwanza ,Jaysam alijeruhiwa mkononi na kutibiwa zahanati ya chuo usiku huo huo.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo Jaysam amemuomba mkuu wa jeshi la polisi Mkoani Mwanza Kamanda Libelatus Baro kwa kushirikiana na Uongozi wa Chuo cha Mtakatifu Agustino kuimarisha Ulinzi maeneo ya Malimbe ambapo idadi kubwa ya wanaoishi maeneo hayo ni Wanafunzi wa chuo kikuu cha  Mtakatifu Agustino, “unajua ulinzi chuoni hapa upo ndani ya chuo kutokana na chuo kuajiri kampuni ya ulinzi ndani ya chuo, lakini sisi wanafunzi tunaoishi nje ambao ni wengi tumekuwa hatuna ulinzi kabisa na hivyo hujikuta tukivamiwa na wahalifu katika hosteli zetu na hata usiku wakati tunatoka chuoni kujisomea”, alisema Jaysam.

Katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, Mwanza karibia robo tatu ya wanafunzi wa chuo hicho zaidi ya 10,000 wanaishi katika hostel za nje ambazo zipo maeneo ya jirani na chuo hicho kutokana na uhaba wa hostel za ndani zinazomilikiwa na chuo hicho. Matukio kama hayo yamekuwa yakiripotiwa kutokea hasa kwa wanafunzi wanaoishi hosteli za nje ya chuo kutokana na ulinzi wa maeneo hayo kutokuwepo hivyo kutoa mwanya kwa wahalifu kufanya uhalifu kwa wanafunzi hao.

Jaysam Jeremiah akiwa katika zahanati ya chuo akisubili kutibiwa jeraha lake baada ya kujeruhiwa katika tukio la uhalifu juzi.

Jraha la kisu alilolipata Jaysam alipokuwa akijitetea baada ya kuvamiwa na wahalifu juzi usiku.

Advertisements

6 responses to “UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA WATISHIA MAISHA YA WANAFUNZI WAISHIO HOSTEL ZA NJE SAUT MWANZA

  1. poleni sana wenzetu mliokutwa na mabalaa hayo, this is scary, The uni’s administration should act quickly in finding ways to tighten up security coz this is now becoming very common around campus. We should be more cautious when walking around at night and better walk around in groups and using main roads.

  2. Duh! Poleni sana ndugu zangu, ninachofikiri hatuna budi kujihami maana hadi huo ulinzi wa polisi uje ufike tutakuwa tumeumia kwa namba kubwa. ”Let us walk in mob in those late hours”

  3. Pole kwa majeruhi….. The university should put effort on out campus security na waziri wa ulinzi nae ashughulikie hili jambo maana naimani hii sio mara ya kwanza kwa hiki kitu kutokea.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s