TUMAINI IRINGA: MKUU WA MKOA ATEMBELEA, AAHIDI KUSHUGHULIKIA TATIZO LA MIKOPO TUIUCO.

Na. Daudi Cholobi, Tumaini Iringa.

Mkuu wea mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma jana alifanya ziara katika Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa (TUIUCo) kwa ajili ya kwenda kusikiliza kilio cha wanafunzi wa chuo hicho juu ya swala zima la kupata fedha za mikopo toka Bodi ya mikopo ya elimu ya juu na kuahidi kulishughulikia tatizo hilo mara moja.

Ziara hiyo ya mkuu wa mkoa katika chuo hicho imekuja mara baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa chuo hicho hasa wa mwaka wa kwanza katika fani ya Uwalimu ambao takribani wote hawajapata fedha zao za mikopo. Akianza kutoa risala fupi katika kikao hicho na mkuu wa mkoa Rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo Bw. Method Kagoma alieleza matatizo yanayowakabali wanafunzi wa chuo hicho ambao wengi ni watoto wa masikini na wanategemea fedha za bodi kuweza kujikimu na hali ngumu ya maisha iliyopo nchini, ukiangalia gharama za kusoma elimu ya juu zinazidi kupanda kila kukicha.

Akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Iringa , mkuu wa wilaya ya Iringa Capt.Asser Msangi  aleleza kwamba serikali ya wilaya na mkoa inavyojitahidi kurekebisha matatizo hayo.

Dk. Ishengoma,mkuu wa mkoa wa Iringa mara baada ya kuwasili chuo kikuu cha Tumaini, Iringa.

Mkuu wa mkoa akiteta jambo na Rais wa serikali ya wanafunzi Bw. Method Kagoma

Rais wa serikali ya wanafunzi Tumaini (TUSO,IUCO), Bw. Method Kagoma akito angalizo kabla ya mkuu huyo wa mkoa kuongea kabla ya kumkaribisha mkuu wa wilaya ya iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Capt.Asser Msangi akimkaribisha mkuu wa mkoa kuongea na wanafunzi.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma akihutubia wanafunzi (Hawapo pichani) wakiokusanyika kwa wingi chuo hapo jana katikati rais wa wanafunzi na kulia ni mkuu wa wilaya.

Baadhi ya sehemu ya wanafunzi waliofika kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa alipokuja kusikiliza matatizo yao hapo jana.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s