CHUO KIKUU MZUMBE: KUCHANGISHA FEDHA

CHUO Kikuu Mzumbe leo kinatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa matayarisho ya shughuli ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuleta uwiano sawa wa jinsia katika chuo hicho.Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, utahudhuriwa na waliopitia chuoni hapo na marafiki wa Mzumbe.

Kati ya wanaotarajiwa kuwepo katika mkutano huu wa matayarisho ya kampeni ya kuchangisha fedha hizo ni wahitimu wa chuo hicho ambao ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Ludovick Utouh, Spika wa Bunge , Anna Makinda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Blandina Nyoni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Chuo Kikuu Mzumbe, Rainfrida Ngatunga kampeni hizo za kuchangisha fedha zinatarajiwa kufanikisha kupatikana Sh4.5 bilioni kutokana na michango ya hiyari kutoka kwa watu binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali.

“Bado kuna fursa zisizolingana zinazotolewa kwa wasichana na wavulana katika nchi yetu,”inaeleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kwamba kuna umuhimu wa kuleta uwiano wa kijinsia.”

Kutokana na kampeni hiyo, Mzumbe inatarajia kujenga hosteli mbili zaidi za wanawake katika kampasi ya Morogoro na mkoani Mbeya.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s