REDD’S UNI-FASHION BASH YAPATA WASHINDI VYUO VYA DAR.

Shindano ya ubunifu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ya REDD’S UNI-FASHION BASH yalifanyika jumamosi ya ya juzi katika ukumbi FPA karibu na CRDB Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambapo washindi wake walipatikana katika shindano hilo huku washiriki wakitoa upinzani mkali na kufanya vitu vikubwa tofauti na ilivyotarajiwa na wengi.

Aidha shindano hilo lililoandaliwa na kinywaji cha REDD’S ORIGINAL lilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba huku likitarajia kufanya maonyesho mengine makubwa katika vyuo vya mikoa mingine mitatu ya Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza.

Washindi wa shindano hilo kwa upande wa Mitindo ni 1. Marvin Peter (Ustawi wa jamii), 2. Benson Macha (CBE), Asha Mohamed (TIU), Yusuph Fanuel (CBE), Aloycia Innocent (UDSM). Aidha kwa upande wa Ubunifu washindi wa kwanza mpaka wa tano ni 1. Jackson Gumbala (UDSM), 2. Esther Amos (CBE), 3. Mirium Kairusi (IFM) na 4.Shabani (UDSM).

Washindi wote walizawadiwwa zawadi zao hapo hapo ukumbini toka kwa waandaji wa shondao hilo Kinywaji cha Redd’s Original, huku burudani kabambe toka kwa wanamuziki Roma Mkatoliki na Joh Makini wakidondosha burudani ya nguvu kwa mashabiki wao.

Washiriki wakiinyesha ubunifu wao jukwaani.

Washiriki wa shindano hilo wakionesha ubunifu na mitindo yao jukwaani.

Hayo ndio mambo yaliyotokea siku hiyo.

Meneja wa kinywaji cha Redd's Original, Victoria Kimaro akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la Ubunifu Bw. Jackson Gumbala kutoka Chuo Kikuu Dar es salaam, mshindi wa kwanza alikabidhiwa kiasi cha shilingi laki saba.

Meneja Uhusiano wa TBL, Bi. Edith Mushi akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa katika upande wa mitindo Marvin Peter kuotka chuo cha ustawi wa jamii, mshindi wa kwanza wa Mitindo alipata jumla ya shilingi laki tano taslimu.

 

Advertisements

One response to “REDD’S UNI-FASHION BASH YAPATA WASHINDI VYUO VYA DAR.

  1. It’s good that you have launched this site or blog.
    This will give a wider range for the young scholars to share their views.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s