SAUT STUDENTS PUBLIC RELATIONS ASSOCIATION WAFANYA SEMINA KWA WANACHAMA WAKE JUMAMOSI.

Wanachama na viongozi wa SAUT STUDENTS PUBLIC RELATIONS ASSOCIATION (SSPRA) jumamosi ya mwisho wa wiki hii walifanya semina ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza na pia kuwakumbusha wanachama wa zamani juu ya kazi na majukumu ya SSPRA katika hali ya kukijenga na kukiimarisha chama hicho semina iliyofanyika katika moja ya madarasa chuoni hapo ndani ya jengo la Mwanjonde.

Aidha akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Kikao hicho ndugu Frank Mashauri alianza kwa kumkaribisha Makamu mwenyekiti wa SSPRA ndugu Wilfred Medard, Bw. Wilfred alianza kwa utambulisho wa Viongozi wa chama hicho pamoja na wajumbe kutoka kamati mbalimbali za chama hicho, ambapo baadae aliweza kutoa malengo na madhumuni ya chama hicho ili kutoa mwanga kwa wanachama wapya kufahamu nini majukumu ya chama hicho.

Akizungumza katika semina hiyo Mlezi wa SSPRA Bw. Albert Tibaijuka ambae pia ni mwalimu wa fani hiyo alielezea historia fupi ya Chama hicho ambapo ilianza kwa Wanafunzi wa Mass Communication waliokuwa wanasoma Public Relations mwaka 2007, Mr. Tibaijuka aliwaeleza wanachama wa chama hicho juu ya upendo, kuheshimiana pamoja na kuwajibika katika kuijenga SSPRA. Akidokeza madhumuni ya Ofisi ya Public Relations kwa mwaka huu Bw. Tibaijuka alisema kuwa Department ya Public Relations ipo katika mchakato wa kuomba Public Relations Laboratory kwa uongozi wa chuo ambayo itatumika na wanafunzi wa Public Relations kufanya shughuli zao za kimasomo, pia department ipo katika mchakato wa kutengeneza kamati ya mahafali ya mwaka huu ikilenga kuandaa sherehe ya pamoja kwa kuangalia miaka 50 ya uhuru na muelekeo mzima wa Public Relations nchini.

Makamu mwenyekiti wa SSPRA Bw. Wilfred Medard kushoto akitambilisha viongozi mbalimbali pamoja na kamati za chama hicho, pembeni kulia ni Frank Mashauri ambae ni mwenyekiti wa kikao hicho.

Wanachama wa SSPRA wakifanya sala ya pamoja kufungua kikao hicho.

www.tzcampusvibe.wordpress.com

Mwenyekiti wa kikao hicho Bi. Upendo Kessy mwanafunzi wa mwaka wa tatu shahada ya Public Relations and Marketing akijitambulisha kwa wanachama kabla ya kumakribisha makamu mwenyekiti kuelezea Maudhui ya Chama hicho.

Baadhi ya wanachama.

Mhazini wa Chama hicho Bi. Zawadi akisikiliza kwa makini semina hiyo.

Kushoto ni mlezi wa SSPRA mwalimu Albert Tibaijuka akiwa na mmoja wa waasisi wa chama hicho Ndg. Msafiri Lawrence mhitimu wa shahada ya Uhusiano wa jamii mwaka huu akijitambulisha katika semina hiyo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s