TAFES SAUT WAFANYA IBADA YA KUWAKARIBISHA MWAKA WA KWANZA.

Jumuiya ya TANZANIA FELLOWSHIP OF AVANGELICAL STUDENTS (TAFES) usiku wa kuamkia jumapili walifanya maombi na tamasha la neno la mungu kwa ajili ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha Mtakatifu Agustino-Mwanza.

Katika tamasha hilo lilihudhuriwa na Mchungaji Debora Ntepa ambae ni mtunzi wa vitabu mabali mbali vya kiroho,alianza kutoa historia fupi ya jinsi alivyookoka, ambapo aliokoka akiwa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya wasichana ya songea na ameanza kumsikia Mungu toka kidato cha tatu.

Katika mahubiri yake alielezea juu ya swala zima la ndoa ambapo alianza kuelezea kuhusu njia sahihi za kijana kuweza kuingia katika ndoa. Njia ya kwanza ni ndoa ya baraka kutoka kwa mungu, Alisema “Ili uweze kuingia kwenye ndoa katika njia nzuri ni lazima uwasiliane na mungu kujua mtu yupi unapaswa kuingia nae kwenye ndoa”. Njia ya pili ni njia ya kumpenda mtu, unaweza kuingia kwenye ndoa kwa sababu umempenda huyo mtu unaetaka kuingia nae kwenye ndoa.

Katika mahubiri hayo mchungaji alisema kuwa mambo yanayowapa vijana tabu katika mchakato mzima wa kuingia kwenye ndoa na wakishaingia kwenye ndoa ni kutomcha mungu, Uchafu wa mwili na roho pamoja na Uwasherati, ambapo alisisitizia kuwa “kuikimbia zinaa kuna mambo mengi kwanza angalia nguo unazozivaa, angalia mazingira unayokwenda, ukaribu uliopitiliza na mtu mwenye jinsia tofauti kwani mvulana akitaka privacy na msichana basi anataka mambo, sabau nyengine ni kukosa washauri sahihi, mfano mzuri ni Amnon mtoto wa Daudi ambae alikuwa na ndugu yake aliyemshauri kwenda kumbaka dada yake, marafiki wengi wanashari kufanya mambo mabaya, Mithali 13.20”.

Kwaya ya TAFES ikiimba nyimbo ya ibada katika Tamasha hilo.

Waumini wakiimba nyimbo za kumsifu Bwana.

Waimbaji na watumishi wa Mungu wakiimba jukwaani.

Mchungaji Debora Ntepa (kushoto) akijiandaa kuweza kupanda jukwaani kutoa mahubiri ya neno la mungu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s