BODI YA MIKOPO: YATUHUMIWA KUPENDELEA WATOTO WA VIGOGO.

Na: Patricia Kimelemeta na Raymond Kaminyoge, Mwananchi.

WAJUMBE wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), wameituhumu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) kwamba inatoa mikopo kwa watoto wa vigogo huku watoto wa maskini wakishindwa kupata fedha hizo na kuishia kuandamana mitaani. Hatua hiyo imekuja, baada ya baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kudai kuwa, kuna ushahidi wa kuaminika wa baadhi ya watoto wa vigogo waliopatiwa mikopo kupitia bodi hiyo bila ya kutimiza vigezo stahiki, jambo ambalo limesababisha kuwapo kwa malalamiko.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam jana, wajumbe hao walisema kitendo kinachofanywa na bodi hiyo ni kinyume na utaratibu wa utoaji mikopo na kwamba, wanashindwa kuzingatia vigezo wanavyotumia vya kutoa kipaumbele kwa watoto wa maskini, yatima na walemavu, badala yake wanawapa watoto wa vigogo wakati uwezo wa kulipiwa na wazazi wao upo.

 “Jukumu la bodi ni kutoa mikopo watoto wenye vigezo, siyo kuwakumbatia watoto wa vigogo wakati wakijua kuwa wanachokifanya ni kinyume na sheria zilizotungwa, kwa sababu wamekuwa watoa mikopo kwa watoto wa vigogo wakati wazazi wao wana uwezo wa kuwalipia,” alisema Kanji Lugola, Mbunge wa Mwibala (CCM).

Lugola alisema kutokana na hali hiyo maandamano hayataisha, badala yake yatasababisha migogoro mikubwa itakayoambatana na maandamano ambayo yatapelekea kuonekana kuwa bodi hiyo imeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.  Alisema HELSB inapaswa kufuata sheria zilizotungwa na Bunge, siyo kufuata utaratibu wa Serikali ambao unaonekana kukwamisha shughuli za utoaji mikopo kwa wanafunzi hao. Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Christowaja Ntinda, alisema kitendo cha kuwapa mikopo watoto wa vigogo na kuwaacha wa maskini, kinachangia kuongezeka kwa migogoro. 

“Tuna ushahidi wa kuaminika wa baadhi ya watoto wa vigogo wanaochukua mikopo ya elimu ya juu wakati hawana vigezo, jambo ambalo limesababisha watoto wa maskini kuandamana kila kukicha, kutokana na hali hiyo tunaomba Serikali kuliangalia suala hilo,” alisema Ntinda. Alisema miezi iliyopita, Rais Jakaya Kikwete aliunda tume ya kuichunguza bodi hiyo ambayo tayari imemaliza kazi yake na kwamba, taarifa yake imekuwa siri, jambo ambalo linazidi kuongeza mashaka katika hilo, kutokana na hali hiyo wameitaka bodi hiyo kutoa taarifa ili wananchi waweze kujua hatua zilizochukuliwa dhidi ya watendaji hao.

Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu, alisema ili bodi hiyo iweze kufanya kazi kwa utaratibu unaokubalika, inapaswa kufuata sheria zilizowekwa ikiwamo kutoa taarifa za mara kwa mara za wanafunzi wanaostahili kupatiwa mikopo hiyo na vigezo vinavyotumika, ili kuondoa malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara.

Advertisements

One response to “BODI YA MIKOPO: YATUHUMIWA KUPENDELEA WATOTO WA VIGOGO.

  1. Itapendeza kama maoni ya kamati yatakuwa yanafanyiwa kazi kuliko wabunge kalalamika mbele ya waandishi tu! HESLB wanashindwa kukiri tu kwamba suala la kutathmini uwezo wa muombaji kiuchumi ni donda ndugu kwao.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s