RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI SAUT ALAZWA ZAHANATI YA CHUO LEO.

Rais wa serikali ya wanafunzi katika chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT)-Mwanza Mh. Cosmas Mataba akiwa katika chumba cha kupumzikia wagonjwa katika zahanati ya chuo iliyopo chuoni hapo. Mh. Mataba alijikuta akikimbizwa katika zahanati hiyo baada ya kukabiliwa na Malaria pamoja na mwili kukosa nguvu asubuhi ya kuamkia leo, ndipo viongozi wa serikali yake kushirikiana na waziri mkuu kuchukua hatua ya kwenda kumfuata nyumbani kwake na kumfikisha katika zahanati hiyo. Mh. Rais huyo alisema kwamba alianza kujisikia vibaya toka usiku wa kuamkia leo lakini asubuhi ilivyofika ndipo hali ilizidi kuwa mbaya na mwili kukosa nguvu hadi kushindwa kuongea, Akizungumza na Blog ya Wanafunzi ya TzCampusVibe Mh. Rais alisema kuwa tangu alivyofika katika zahanati hiyo amekuwa akijisikia vizuri baada ya matibabu aliyoyapa. Aidha anawashukuru wale wote waliofika katika zahanati hiyo kumjulia hali na kwa wale waliomtakia afya njema kwa njia ya simu na kuwaambia wananchi wake kwamba hali yake itakuwa nzuri kabisa na kurudi ofisini kuendelea na kazi jumatatu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s