TCU KUVIPANDISHA HADHI VYUO VIKUU VISHIRIKI VYA TUMAINI

Bodi ya Ithibati ya Vyuo vikuu Tanzania, iko katika hatua za mwisho ya kuvipa hadhi ya kuwa vyuo vikuu kamili vinavyojitegemea, Chuo Kikuu cha Iringa (IUCo), Chuo Kikuu cha Tiba cha KCMC na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Sebastian Kolowa (SEKUCo). Vyuo hivyo kwa sasa ni vyuo vikuu vishiriki vya Chuo Kikuu cha Tumaini-Makumira kilichopo mkoani Arusha.

Hatua hiyo ya kufanyika kwa mabadiliko chanya ya Chuo Kikuu cha Tumaini,yalitangazwa jana na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Alex Malasusa katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu cha Iringa. Akisoma taarifa hiyo kwa niaba yake, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Joseph Parsalaw, alisema wamewasilisha katika Bodi hiyo, mapendekezo na viambatisho vya maamuzi yaliyofikiwa na Kanisa hilo katika kuviboresha vyuo vyake.

“Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kimeshawasilisha charter na viambatisho vyake serikalini kupitia Bodi ya Ithibati ya Vyuo Vikuu Tanzania, tunakichokisubiri kwa sasa ni hiyo charter kusainiwa…Kanisa limekubaliana na vyuo vya Iringa (IUCo), KCMC na SEKUCo kwamba viwe ni vyuo vikuu vinavyojitegemea, ’’ alisisitiza.

Kwa mujibu wa Profesa Parsalaw, mabadiliko hayo katika Chuo Kikuu cha Tumaini yalifikiwa Agosti 5, mwaka huu.

Vyuo vingine ambavyo ni vyuo vikuu vishiriki vya Tumaini ni pamoja na Chuo cha Tumaini Dar es Salaam (TURDACo),Chuo cha Kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMMUCo),Chuo cha Kumbukumbu ya Joseph Kibira (JOKUCo) na Chuo cha Pamoja (SUCo) na SHUCo.

Katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Profesa Esther Mwaikambo, aliwatunuku astashahada, stashahada, shahada na shahada ya uzamili,wahitimu 1,062 wa chuo hicho.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s