MAHAFALI CHUO CHA TUMAINI DAR LEO: Askofu- Siasa zinawavuruga wanafunzi vyuoni

Wahitimu wa Shahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, tawi la Dar es Salaam, wakisubiri kukabidhiwa vyeti vyao wakati wa Mahafali ya Tano ya Chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam.

ASKOFU Mkuu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Elinaza Sendoro, amesema changamoto kubwa inayowakabili wanataaluma nchini hivi sasa ni kuwapo watu wanaoingiza siasa vyuoni na kuvuruga wanafunzi. Askofu Sendoro alisema hayo Dar es Salaam jana kwenye mahafali ya tano ya Chuo Kikuu cha Tumaini tawi la Dar es Salaam (TUDARco), ambapo jumla ya wanafunzi 744 walihitimu na kutunukiwa vyeti.

Alisema baadhi ya watu wamekuwa wakiingiza siasa kwa wanafunzi vyuoni kwa kila jambo, tena kwa ushabiki, ili wapate kuungwa mkono na kupata nguvu, jambo ambalo alisema halifai, kwani kufanya hivyo ni kuwapoteza wanafunzi.  “Tusichomekee siasa

kwenye taaluma, tuwape wanataaluma nafasi na wahitimu watumie taaluma waliyopata kushauri watu wanaoingiza siasa vyuoni, ili kupunguza ushabiki ambao utavuruga wanafunzi,” alisema.

Pia alizungumzia changamoto za ajira kwa wahitimu vyuoni, kwamba wanachelewa kupata ajira, hivyo kuhimiza kuwa wasitarajie kuajiriwa tu, bali pia watafute fursa ya kujiajiri wenyewe, ili kupambana na changamoto za kimaisha.  Alisema ingawa katika fani nyingine kuna ugumu katika kujiajiri, kuna umuhimu wa chuo hicho kuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuhitimu, ili wanapoingia mitaani wasitarajie kuajiriwa na badala yake waje na mbinu zitakazosaidia katika harakati za kujikomboa kama ilivyo kwa vyuo vingine.

Aliwahimiza wanasheria wanaohitimu, kujiunga na vikundi vya kutetea haki za wananchi, ambao wamekosa haki zao kwa vile hawajui sheria ili hatimaye waweze kurudishiwa haki zao. Alisema idadi ya mawakili nchini ni 2,001 ambao ni wachache ikilinganishwa na nchi zingine, hivyo kusisitiza umuhimu wa kuongeza idadi ya wahitimu wa sheria ili waajiriwe kwa wingi kwa lengo la kusaidia wananchi kutetea haki zao.

Mkuu wa Chuo cha TUDARco, Profesa Geofrey Mmary, alisema Chuo kilianzisha kozi mpya mapema mwaka huu, ambazo ni za cheti cha sheria, ualimu na masomo ya muda mfupi kwa watumishi wa Dayosisi.

Katika mahafali hayo wanafunzi 38 walihitimu Cheti cha Udhibiti Kumbukumbu, 52 Shahada ya Ukutubi na Taaluma ya Habari, 148 Shahada ya Sanaa ya Mawasiliano ya Umma, 133 Cheti cha Uhasibu na Uendeshaji wa Biashara, 109 Uendeshaji wa Biashara na 265 Shahada ya Sheria.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s