KUTOKA SAUT: MASHINDANO YA PRO-LIFE YAANZA RASMI LEO.

Mashindano inayohusisha wanafunzi wa SAUT inayojulikana kama PRO-LIFE imeanza kutimua vumbi leo hii katika viwanja vya Raila Odinga  SAUT-MWANZA ikishirikisha michezo mbalimbali. Katika mchezo wa mpira wa miguu leo hii mechi ya kwanza ilikuwa ni katika ya wanafunzi wanaugavi (Procurement) dhidi ya wanasheria (LLB) ambapo timu ya wagavi ilijikuta ikiwaduwaza wanasheria kwa kuchapo cha 2-1 ambapo mchezaji mmoja wa timu ya wanasheria akipewa kadi nyekundu baada ya kucheza rafu mbaya. Mechi ya pili iliwakutanisha miamba ya soka miwili kati ya Walimu (EDUCATION) na wafanya biashara (BBA) ambapo mchezo huo uliokuwa mkali ulishuhudia timu zote zikitoshana nguvu ya bila kufungana mpaka kipenga cha mwisho cha muamuzi kinapulizwa.

Mechi za kesho ni BAPRM VS TOURISM saa 8.00 mchana na inayofuata ni MASS COMMUNICATION Vs CERTIFICATE saa 10.00 Alasiri.

Matukio ya Michezo hiyo Pichani.

Timu ya soka ya BBA.

Timu ya soka ya Education.

Ilikuwa ni hekaheka katika goli la BBA waliovaa jezi nyekundu.

Mashabiki wakiwa tayari kushuhudia michuano hiyo.

Brki mahiri wa Timu ya BBA akimsaidia kiungo wake ambae leo alionesha mambo makubwa kwa pasi za uhakikka katika mchezo huo.

Kulikuwa na burudani ya Ngoma ya asili wakati wa mapumziko.

Viduku vya Kisukuma navyo vilikuwepo..

Iki nacho kilikuwa kituko kingine..huyu bwana ni shabiki mkubwa sana wa Edecation na ni Mwalimu mtarajiwa hapa alikuwa ameshapiga yale mambo yake akiwaambia wanafunzi wa Mahusiano ya jamii (BAPRM) kwamba anawaitaji, mechi yao kati ya BAPRM na Edecation ni wiki ijayo.

KWA UPANDE WA VOLLEYBALL MAMBO YALIKUWA HIVI.

KWA UPANDE WA NETBALL TIMU YA PUBLIC RELATIONS (BAPRM) IMEWAFUNGA WENZO WA EDUCATION KWA MAGOLI 14-8.

Madada wa timu ya Public Relations wakati wa mapumziko.

Huyu dada kama pale Barcelona unaweza ukasema Messi, maana yeye alikuwa anatupia tu, Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Public Relations.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s