KUTOKA NATIONAL INSTITUTE OF TRANSPORT (NIT): MOTO WATEKETEZA JENGO.

Baadhi ya wafanya kazi wa National Institute of Transport (NIT) wakikusanya mabaki ya vitu baada ya moto uliozuka usiku majira ya saa 3:00 kuteketeza jengo lenye ofisi za uhasibu na bohari, Mabibo Dar es salaam. (Picha na Robert Okanda)

MOTO uliozuka usiku wa kuamkia jana umeteketeza jengo lenye ofisi za uhasibu na bohari katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.  Mkuu wa chuo hicho, Zakaria Mganilwa alisema moto huo uliogunduliwa na wanafunzi wa
chuo hicho, ulianza majira ya saa tisa usiku.

Mganilwa alisema jengo la uhasibu zimeteketeza nyaraka zote za uhasibu za chuo hicho, ikiwa ni pamoja na kompyuta saba zilizokuwa zikitumiwa katika kuhifadhi hesabu za chuo. Alisema kwa upande wa bohari, waliweza kufanikiwa kuokoa vitu vichache ambavyo pia haviko katika hali nzuri.

Baadhi ya vitu vilivyoteketea kwenye bohari ni pamoja na jenereta za tahadhari nne, seti tatu za televisheni za ukubwa wa inchi 42 na kompyuta ndogo 12 aina ya Lap Top. Alipoulizwa kuhusu chanzo cha moto huo, Mganilwa alisema “ Ni ngumu sana kueleza chanzo
cha moto huo, lakini Katibu Mkuu (Wizara ya Uchukuzi) ameunda tume ambayo itachunguza
chanzo cha moto na kutathimini hasara kamili ya mali zilizoteketea.” Kwa upande wa polisi, Kamanda wa Kinondoni Charles Kenyela alisema bado wanafanya uchunguzi wa moto huo.

Advertisements

One response to “KUTOKA NATIONAL INSTITUTE OF TRANSPORT (NIT): MOTO WATEKETEZA JENGO.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s