KUTOKA SJUT DODOMA: PINDA ALONGA, CHUO KUIMARISHA MAFUNZO YA MASOMO YA SHAHADA YA FAMASIA.

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wazazi wenye uwezo wa kulipia watoto wao katika Vyuo Vikuu waache kusema uongo kwani kwa kufanya hivyo wanawakosesha watoto wa masikini kupata mikopo wanayostahili. Ametoa kauli hiyo wakati akiwahutubia washiriki wa mahafali ya pili ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St. John’s) yaliyofanyika kwenye chuo hicho mjini Dodoma.

Jumla ya wahitimu 1,002 walitunukiwa vyeti, stashahada, shahada na stashahada za juu katika fani za theolojia, uuguzi, famasia, sayansi na ualimu, biashara, uhasibu na fedha, masoko na teknolojia ya habari na mawasiliano. “Bado kuna malalamiko nayapata kupitia njia mbalimbali kuhusu utaratibu wa Bodi ya Mikopo hasa pale watoto wa maskini, tena waliofaulu vizuri wanapokosa mikopo. Nawasihi wazazi wenye uwezo waache kusema uongo kwa sababu si busara kuwatumia watoto wao kupata mikopo wakati watoto wanaostahili wanaikosa…,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuzungumzia changamoto zinazoikabili Serikali katika kukabiliana na kasi ya ongezeko la watu na kuonya kuwa linaleta changamoto kubwa katika utoaji wa huduma za jamii. Akitoa wosia kwa wahitimu, Waziri Mkuu alisema: “Ombi langu kwenu ni kuwa, mkatumie elimu mliyoipata hapa chuoni kwa manufaa yenu, jamii na Taifa kwa ujumla.

Msianze kwa kujifikiria nafsi zenu, kwani huo ni mwanzo wa tamaa, uchoyo, dhuluma, rushwa
na pengine wizi.” ”Kwa sasa wapo Watanzania wengi wanajifikiria wenyewe, wamekuwa na tamaa hasa ya mali bila kuwafikiria Watanzania wenzao. Uzalendo unapungua. Hili naweza kusema ndilo chimbuko la maovu yaliyomo kwenye jamii yetu kama wizi, rushwa, ufisadi na hata mauaji yakiwemo mauaji ya walemavu wa ngozi. Kwa mwenendo huu hatuwezi kusonga mbele kiuchumi wala kijamii. Tunahitaji kubadili mwelekeo. Nanyi ni wadau muhimu katika kubadili mwelekeo wa jamii yetu,” aliwaasa.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wahitimu hao, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Balozi Paul Rupia alisema Chuo hicho kina mpango wa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Afrika Kusini katika kuimarisha mafunzo ya shahada ya famasia. Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eginald Mihanjo alisema hii ni mara ya kwanza kwa chuo hicho kutoa Shahada ya Uuguzi na Famasia. Waliohitimu uuguzi ni 150 na famasia ni 29.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s