KUTOKA UDOM: BAADHI YA MASOMO KUFUNDISHWA KWA NJIA YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO.

KATIKA kuhakikisha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) hawaathiriki na upungufu wa wadhahiri, chuo hicho kinakusudia kuanzisha mpango wa kufundisha baadhi ya masomo kwa njia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama), kikiunganishwa na vyuo vingine kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Hayo yalielezwa jana mjini hapa na Mwenyekiti wa UDOM, Balozi Juma Mwapachu alipotembelea chuo hicho, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo, akiziba nafasi iliyoachwa na Dk. Mohamed Gharib Bilal ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Balozi Mwapachu alisema kuwa ili kukabiliana na upungufu wa wahadhiri ni vyema kwa vyuo
vikuu vya Afrika Mashariki kwa kutumia mkutano wa njia ya Video katika kufundisha, ili viweze kukidhi mahitaji ya wanafunzi wa vyuo vikuu vyote vya Afrika Mashariki kuliko kuendelea kulalamika kuwa vyuo vina uhaba wa wahadhiri.

Alisema sasa chuo kinasubiri matengenezo ya mkonga wa taifa wa mawasiliano ukamilike chuoni hapo ili waangalie uwezekano wa mhadhiri mmoja kufundisha kwenye vyuo zaidi ya vitano vilivyoko ukanda wa Afrika Mashariki. “Tatizo la upungufu wa wahadhiri linaweza kutatuliwa kwa mikutano kwa njia ya video, kwa
hivi sasa tunaangalia uwezekano wa mhadhiri mmoja kufundisha somo moja kwa vyuo zaidi ya vitano kutumia mkonga wa mawasiliano ili tuweze kuunganisha chuo chetu na vyuo vingine
Afrika Mashariki,” alisema Mwapachu.

Alisema kuwa anaangalia uwezekano wa kukiunganisha chuo kikuu cha Dodoma na vyuo vikuu vingine vya Kenya, Uganda Rwanda na Burundi. Alisema kuwa faida mojawapo ya kutumia njia hii ni pamoja na kupunguza safari za wanafunzi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ya nchi kwa ajili ya kutafuta mwalimu wa somo
ambalo analisomea kama vile udaktari.

Vilevile aliwaasa wanafunzi kuacha kutumia migomo vyuoni kama njia ya kutatua matatizo yao, bali watumie mazungumzo zaidi ili kuleta mafanikio na tija katika masomo yao. Mwapachu ambaye hivi karibuni alimaliza muda wake wa kuwa Katibu Mkuu wa EAC, alitembelea Kitivo cha Sayansi na Tiba, Sayansi ya Ardhi, Sayansi ya Hesabu, Kituo cha Utafiti cha Dk. Asha-Rose Migiro pamoja na ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka yanayotoka chuoni hapo.

Advertisements

One response to “KUTOKA UDOM: BAADHI YA MASOMO KUFUNDISHWA KWA NJIA YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s