KUTOKA UDSM: WANAFUNZI KUFANYA BONANZA KUBWA NOVEMBA 12 HOSTELI ZA MABIBO.

Baaadhi ya majengo ya Hostel za Mabibo wanapoishi baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Bonanza hilo litafanyika katika viwanja vya Hostel Hizi.

ZAIDI ya wanafunzi 100 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Novemba 12 mwaka huu watashiriki katika bonanza kubwa la michezo litakalofanyika katika viwanja vya Hosteli ya Mabibo. Akizungumza katika ofisi za gazeti hili Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam upande wa wanafunzi, Prisca Lawrence alisema tamasha hilo litakuwa la aina yake na linatarajia kushirikisha zaidi ya wanafunzi 100 wa chuo hicho.

Lawrence alitaja michezo itakayoshindaniwa kuwa ni pamoja na mpira wa miguu, riadha, kukimbiza kuku, kukimbia na yai, kushindana kunywa soda kwa haraka na michezo mingine kibao. Alisema pamoja na mambo mengine lengo kuu la bonanza hilo ni kuwawezesha wanafunzi hao kujumuika pamoja katika michezo.

Alisema bado wanasaka wadhamini mbalimbali ili kufanikisha bonanza hilo, ambalo ni muhimu kwa ajili ya kuwakutanisha wanafunzi tofauti tofauti. Alisema bonanza hilo ambalo litawashirikisha wanafunzi wakike na kiume, washindi katika michezo mbalimbali watazawadiwa zawadi za aina tofauti, ambazo hata hivyo hakuzitaja, lakini alisisitiza kuwa zitakuwepo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s