KUTOKA SAUT: MASHINDANO YA PRO-LIFE YAENDELEA TENA HII LEO.

Mashindano ya PRO-LIFE yameendelea tena hii leo ikishuhudiwa michezo miwili kwa upande wa mpira wa miguu ikichezwa katika viwanja vya Raila Odinga. Mechi ya kwanza ni ile kati ya Timu ya Mahusiano ya jamii (BAPRM) iliyokuwa ikimenyana na timu ya TOURISM, katika mchezo huo wanamahhusiano ya jamii waliibuka kwa ushindi mnono wa 6-0.

Aidha katika mchezo mwengine ulioanza majira ya saa kumi alasiri ulikuwa ni kati ya timu ya Mawasiliano ya Umma (BAMC) dhidi ya muunganiko wa madarasa ya CERTIFICATE ambapo waandishi wa habari leo hii walijikuta wanatoka uwanjani vichwa chini baada ya kutandikwa bila huruma 2-1. Walikuwa ni wanahabari walionza kujipatia goli mnamo kipindi cha kwanza lilofungwa na mshambuliaji wao Kedmund Vicent ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamaliza matokeo yalikuwa ni 1-0. Aidha mambo yalibadilika kipindi cha pili pale vijana wa Cheti walipokuwa juu kwa kulisakama lango la Wanahabari na  ndipo ilipojipatia goli la kusawazisha kupitia kwa Pheremon Kulwa kabla ya beki wao mashuhuri Kelvin Kilua kupachika goli la pili kwa faulo safi.

MATUKIO YA MICHEZO HIYO PICHANI.

Kigoma cha Public Relations nacho kilikuwepo..ilikuwa ni mwendo wa PR PR PR PR PR...

Mashabiki wa PR wakitoa burudani kwa kucheza style ya kisauzi..

Wachezaji pamoja na mashabiki wa PR wakimshukuru mungu kwa ushindi baada ya kumalizika kwa mchezo wao.

Mashabiki wa PR wakishangilia ushindi.

Kutoka kulia ni mdau Mkumba Iddi (Kisiga), Raymond Mwakihaba CR wa PR mwaka wa tatu (katikati)na Azizi wakishuhudia mchezo huo...

MATUKIO YA MECHI KATI YA MASS COMM VS CERTIFICATE.

Ilikuwa ni hatari katika lango la Mass Communication.

Wachezaji wa Mass Communication wakipongezana baada ya kuandika bao la kwanza..kabla ya kujua nini kitafuata mbele yao..

Ilikuwa bora lawama kuliko fedheha..Mshambuliaji wa Mass Communication Kedmund Vicent akijaribu kupiga cross mbele ya beki wa Certificate.

Timu zikaenda mapumziko..Mass Comm wakiongoza 1-0..

Waamuzi nao wakiwa kwenye mapumziko..

Kipindi cha pili kikaanza..Wachezaji wa Cheti wakiwa tayari kuanza.

Cheti wakashangilia goli la kwanza la kusawazisha.

Msuli wa mguu ulileta tabu kidogo.

Cheti wakashangilia goli la pili.

Mwisho wa siku Waandishi wa Habari wakamshukuru Mungu kwa walichokivuna.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s