KUTOKA SAUT-STUDENTS ORGANISATION: KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI CHAFANYIKA JIONI YA LEO.

Baraza la mawaziri la serikali ya wanafunzi SAUT likikaa chini baada ya kuomba dua ya pamoja kufungua kikao hicho leo kilichofanyika katika Canteen iliyopo chuoni hapo, Baraza hilo lilikaa leo kujadili utendaji mzima wa serikali hiyo kwa kujadili mafanikio na changamoto za kila wizara. Pia baraza lilijadili kuhusu mkutano mkubwa wa kimataifa unaoandaliwa na serikali hiyo ya wanafunzi ya SAUT utakaoshirikisha wanafunzi wa vyuo vya nchi za ukanda wa Afrika mashariki utakaofanyika jijini Mwanza 16 mpaka 18 mwezi huu na ajenda ya tatu ilikuwa ni kuhusu faini ya laki moja wanayotozwa wanafunzi wa SAUT wanaochelewa kusajiliwa bila ya sababu maalum.

Mh. Rais wa Serikali ya wanafunzi Katika Chuo cha Mtakatifu Agustino, Mh. Mataba Cosmas akifungua mkutano huo wa Baraza lake la mawaziri jioni ya leo hii.

Mh. Waziri wa Mikopo, Mh. Yaredi akitoa taarifa ya mafanikio na changamoto za wizara yake katika kikao hicho. Wizara ya mikopo ni moja kati ya wizara zenye mafanikio katika shughuli zake za kuwatumikia wananchi wake hasa kwenye swala la zima la watu kupata mikopo yao.

Mh. Waziri wa Michezo, Bw. Kadutu nae akitoa taarifa ya mafanikio na Changamoto za wizara yake, Ambapo mafinikio ni kutengeneza timu bora ya chuo yenye ushindani, usimamizi wa fedha za mashindano yanayofanyika chuoni hapo, ukarabati wa viwanja vya michezo chuoni hapo, usimamizi mzuri wa ligi na mashindano mbalimbali ya chuo, uwandaaji wa matukio ya burudani kwa wanafunzi kama Bon fire na Galla Night ambapo walifanikiwa kuwaleta wasanii kama Cpwaa na Roma Mkatoliki.

Mh. Waziri wa Chakula, Bw. Priscus Mushi akitoa taarifa juu ya mafanikio na changamoto za wizara yake katika swala zima la upatikanaji wa chakula chuoni hapo.

Mh. Rais wa serikali ya wanafunzi (wa pili kutoka kulia) Mh. Cosmas Mataba, kushoto wa kwanza ni Mh. Makamau wa Rais Bi. Anna Mushi, anaefuata ni Mh. Katibu wa Rais, Kutoka kulia ni Mh. Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi Leonard Mafuru,wakiwa katika mkutano huo wa baraza la mawaziri.

Mh. Waziri Mkuu, Bw. Leonard Mafuru akitoa majumuisho ya utendanji wa wizara mbalimbali.

Mh. Makamu wa Rais Bi. Anna Mushi akitoa maneno yake juu ya utendaji kazi wa baraza la mawaziri.

"Tuupigieni kura Mlima Kilimanjaro uweze kushinda nafasi ya kuwa moja kati ya maajabu saba ya dunia" Mh. Rais akiwakiwakumbusha watendaji wake kuupigia kura mlima Kilimanjaro.

Hatimae baraza mawaziri lilihitimisha kikao chake saa nne za usiku toka saa kumi na moja kwa dua.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s