KUTOKA BUNGENI: Gharama za elimu vyuo kikuu zatafutiwa mtaalamu

Mh. Waziri wa Elimu na Ufundi Stadi, Dk. Shukuru Kawambwa.

SERIKALI inatarajia mwezi huu kumpata mtaalamu mwelekezi kwa ajili ya kuangalia gharama za kumsomesha mwanafunzi Chuo Kikuu nchini. Hayo yalielezwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina(CCM) aliyehoji kwa nini serikali haiweki viwango vya ada vinavyofanana kwa vyuo vikuu.

Kwa mujibu wa Mpina, Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) kinatoza Sh 950,000 kwa mwanafunzi anayechukua sheria, lakini kwa anayesomea Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam analipwa Sh milioni 1.5. Kawambwa alisema serikali imeliona hilo na kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wanamtafuta mtaalamu mshauri na lengo ni serikali iweze kupanga viwango sawa vya ada.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Sara Msafiri (CCM) aliyetaka kufahamu kiasi cha fedha ambacho serikali iliwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu tangu kuanza kwa mpango huo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema Sh bilioni 811.3 zimekopeshwa tangu mwaka 1994. Kati ya hizo Sh bilioni 106.3 zipo tayari kuanza kurejeshwa kutoka kwa wanafunzi 69,143 ambao wamehitimu masomo yao na muda wa matazamio umepita.

Alitaja mikakati ya kukusanya madeni ya mikopo kuwa ni kuidhinisha kupitiwa kwa muundo wa Bodi ya Mikopo na kuongeza nafasi za watendaji katika idara ya urejeshwaji mikopo. Kwa mwaka 2011/2012 bodi itaajiri wafanyakazi wapya 12 katika idara ya urejeshwaji mikopo. “Bodi itaimarisha huduma za kukusanya mikopo kwa kutumia wakala wa ukusanyaji mikopo na kuimarisha elimu kwa umma na kuwachukulia hatua za kisheria wadau ambao hawatimizi wajibu wao kikamilifu,” alisema.

Mikakati mingine ni sheria ya bodi kurekebishwa kuiwezesha kupata taarifa za waajiri na waajiriwa na wafanyabiashara kutoka kwa wadau kama mifuko ya Pensheni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na utoaji wa vitambulisho vya uraia ambapo waliokopeshwa watabainika walipo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s