WANAVYUO 15,000 KUKESHA VIWANJA VYA LEADERS.

ZAIDI ya vijana 15,000 kutoka vyuo vya elimu ya juu vya nchini na nje ya nchi wanakutana kushiriki mkesha wa siku moja katika viwanja vya Leaders’ club jijini Dar es Salaam wenye dhumuni la kuwajengea maadili mema. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mchungaji wa Kanisa la Victory Christian Centre lililoandaa mkesha huo, Dk. Huruma Nkone, alisema wanalenga pia kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa kubadilishana mawazo.

Kwa mujibu wa Dk. Nkone, mkesha huo utakaofanyika katika viwanja vya Leaders, ni la sita kufanywa na kanisa hilo. Licha ya mkesha kuwalenga wanafunzi wa vyuo jijini Dar es Salaam, pia utahudhuriwa na baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vya Mzumbe na Sokoine vya mkoani Morogoro wataokuja kama wageni waalikwa. Nkone alisema mkesha huo utahudhuriwa pia na ugeni wa wanafunzi kutoka Kenya, Rwanda, Uganda, Sweeden Afrika Kusini pamoja na Marekani.

Alisema mkesha huo unaofahamika kama ‘Campus Night’, tangu uanze umeleta mabadiliko makubwa kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwafanya wawe na uzalendo kwa taifa lao. “Katika usiku huo, pia tutawahamasisha vijana wote wataohudhuria, kuupigia kura Mlima Kilimanjaro ili uweze kushinda na kuingia katika moja ya maajabu Saba ya Dunia, na hili tutalifanya kabla ya muda wa zoezi la upigaji kura kufungwa rasmi,” alisema Dk. Nkone.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s