UDSM KIMENUKA: WANAFUNZI WAANDAMANA KUDAI FEDHA ZAO ZA MIKOPO KWA AJILI YA MALAZI NA CHAKULA.

Askari wa kutuliza ghasia wakielekea Ubungo ambapo wanafunzi wa UDSM hasa wa mwaka wa kwanza walikusanyika katika maandamano yenye lengo la kuishinikiza bodi ya mikopo kuwapatia fedha zao kwa ajili ya chakula na malazi.

Gari la polisi lenye maji ya kuwasha likielekea kudhibiti maandamano hayo.

Wanafunzi wa UDSM, Hapa ni Academic bridge.wanafunzi wakijadili baada ya kuvurugwa maandamano yao, hata hivyo wameapa kujipanga na kuendelea baadaye.wanaandamana kuhusu kudai mikopo ya mwaka wa kwanza ambao hadi sasa hawajapewa pesa ya chakula wala malazi.

Advertisements

3 responses to “UDSM KIMENUKA: WANAFUNZI WAANDAMANA KUDAI FEDHA ZAO ZA MIKOPO KWA AJILI YA MALAZI NA CHAKULA.

  1. Siku hizi migomo imeenea hapa nchini, kila kona ya nchi ni maandamano. Ushirikiano huu umeanza kutia mashaka kwamba kwa baadaye nchi haitatawalika, Mungu wangu! Mimi nashauri matatizo yanayoweza kuchochea migomo yashughulikiwe mapema.

  2. Ni vema serikali ingetoa tamko ambalo lingeonesha hatima ya wanafunzi hawa ambao wamekosa mikopo kutokana na ufinyu wa bajeti badala ya kuiachia jukumu HESLB ambayo nayo haina majibu ya kistaarabu kwa wadau, kwa mfano wanafunzi hawa wangeweza kuambiwa kuwa kwa sababu bajeti imefika mwisho vyuo mlivyodahiliwa vitatunza nafasi zetu mpaka mwakani nayo bodi ya mikopo itaanza kuwapatia ninyi mikopo kabla ya waombaji wengine wapya, nadhani majibu kama haya yangetia moyo kuliko kukimbizana na mabomu ambayo yatatuliza ghasia tu lakini hayatatatua tatizo. Ni mtazamo wangu

  3. unajua hii serikali fedha za posho za wabunge wanazo sasa wanaona kutoa mikopo ambayo ss wanafunzi tutajairudisha wanaona ni kazi sasa kwa nini tusiandamane??? mimi nachoona ni bora ss wanachuo next election embu tupige kura na tubadili chama kabisa kisiingie hikhiki maana tumewavumilia tumechoka sasa.kikubwa maandamano hadi fedha zetu tupewe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s