MWANAFUNZI TUMAINI APANDISHWA KIZIMBANI KWA UTAPELI.

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Rashid Ramadhan (24), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mashitaka ya kujipatia Sh milioni 15 kwa njia za udanganyifu. Mbele ya Hakimu Mkazi, Warialwande Lema, Wakili wa Serikali Leonard Chalo alidai mwanafunzi huyo alitenda makosa hayo kati ya Januari 19 na Machi mosi, mwaka huu eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Katika mashitaka hayo, alidaiwa kula njama ya kutenda kosa la kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu. Mbali na njama, pia alidaiwa kuwa kati ya Januari 19 na Machi mosi, mshitakiwa huyo alijipatia Sh milioni 15 kutoka kwa Dickson Chacha baada ya kujifanya anakwenda kulipia gharama ya kontena la bidhaa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mshitakiwa pia alidaiwa kuahidi angezirudisha fedha hizo baada ya kuuza bidhaa hizo wakati akijua si kweli. Mshitakiwa huyo alikana mashitaka hayo na alirudishwa rumande baada ya kukosa dhamana. Upelelezi bado haujakamilika na kesi itatajwa Novemba 23 mwaka huu.

HABARI LEO.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s