MGOMO UDSM: WANAFUNZI 41 WAKOSA DHAMANA, WASOTA RUMANDE.

Picha ni kutoka maktaba yetu. Wanafunzi wa UDSM wakiandamana.

WANAFUNZI 41 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana walirejeshwa rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana katika kesi inayowakabili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kukaidi amri ya jeshi la Polisi. Awali wanafunzi 50 wa chuo hicho walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema.

Washitakiwa hao walisomewa mashitaka na waendesha mashitaka mawakili wa Serikali, Ledislaus Komanya na Shadrack Kimaro. Komanya alidai kuwa Novemba 11 mwaka huu, katika eneo la Mlimani, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja walifanya mkusanyiko usio wa halali na kusababisha uvunjifu wa amani katika eneo hilo. Kosa la pili wakili Komanya alidai washitakiwa hao wakiwa kwenye mkusanyiko huo haramu kwa lengo la kufanya mgomo, askari wa jeshi la Polisi waliwazuia na kuwaambia watawanyike lakini walikaidi amri hiyo.

Washitakiwa hao walikana mashtaka hayo na Hakimu Lema alisema ili mshitakiwa apate dhamana, kila mmoja anapaswa kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika ambaye atasaini bondi ya Sh milioni moja. Hata hivyo ni washitakiwa tisa tu kati ya 50 ndiyo waliotimiza masharti na kupata dhamana na wengine walipelekwa gerezani kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Washitakiwa waliopata dhamana ni Rehema Mnuo, Glory Masawe, Happy Amulike, Elisia Mpangala, Frida Timoth, Stela Msofe, Betwel Martin, Mmasi Stephano na Rugemalila Venance. Baadhi ya waliokosa dhamana ni pamoja na Mwambapa Elias, Everest Ambrose, Baraka Monas, Helen Moshi, Alphonce Lusako, Matrona Babu, Rolanda Wilfred, Godfrey Derogations, Moris Denis, Evon Gumbi.

Wengine ni Lugiko Mathias, Ndimbo Jabir, Evarist Wilson, Cornel Rwaga Mushi, Mlazi Kumbuka, Rehema Munuo, Glory Masawe, Happy Amulike, Elias Mpangala, Frida Timothy, Stella Mofe, Betwel Martin, Mmasi Stephen na Lugemalila Venance. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 28 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya upande wa mashitaka kusoma maelezo ya awali baada ya jana kudai kuwa uchunguzi wao umekamilika. Novemba 11 mwaka huu, wanafunzi wa chuo hicho walianzisha mgomo kwa kile walichodai ni kuishinikiza bodi ya Mikopo iwapatie mikopo baadhi ya wanafunzi wenzao ambao walikosa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s