KUTOKA SAUT: WANAFUNZI WA MAHUSIANO YA JAMII WAFANYA SHEREHE YA PAMOJA USIKU WA JANA KATIKA UKUMBI WA NYUMBANI HOTEL, MWANZA.

Wanafunzi wa Shahada ya Mahusiano na Masoko katika Chuo cha Mtakatifu Agustino , Mwanza usiku wa kuamkia leo wamefanya sherehe ya pamoja katika kukaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza na kusheherkea ushindi wa pili waliyoupata katika michuano ya chuo hicho inayojulikana kama FAWASCO kwa msimu uliopita.

Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa ni Mhadhiri wa chuo hicho Emanuel Silaa amae aliwataka wanafunzi hao kupendana na kuheshimiana katika kuleta umoja kwa wanafunzi wote wa program hiyo. Katika sherehe hiyo pia kulikuwa na ugeni kutoka serikali ya wanafunzi ya katika chuo hicho ambapo Rais wa serikali ya wanafunzi Mh. Cosmas Mataba pamoja na Waziri mkuu Mh. Leonard Mafuru walipata fursa ya kuwakilisha serikali hiyo ya wanafunzi.

Kutoka kushoto ni Mhadhiri wa chuo hicho kitengo cha Public Relations Gibson, Rais wa serikali ya wanafunzi Cosmas Mataba, Mgeni rasmi Emanuel Silaa pamoja na Waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Leonard Mafuru wakiwa meza kuu.
Mgeni Rasmi katika sherehe hizo akitoa nasaha zake kwa kusiisitizia swala la umoja kwa wanafunzi wote wa program hiyo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s