AJALI YA TAQWA KAGERA: WANAFUNZI SITA UDSM WAFA.

Nshaija Muganyizi, Tanzania

Kassim Dadi - Tanzania

Chimuka Hamajata - Zambia

Chikondi Chasowa - Malawi

Josephine Kaleso - Malawi

Mubiru Patrick - Uganda

WANAFUNZI sita waliokuwa wakisoma Shahada ya Uzamili, Hisabati katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni miongoni mwa watu 18 waliokufa Jumamosi katika ajali ya basi la Taqwa lililogongana na lori mkoani Kagera. Kwa mujibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, marehemu hao ni miongoni mwa wanafunzi 10 wa UDSM waliokuwa wakienda Kigali nchini Rwanda kwa ajili ya ziara ya kimasomo katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Kigali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Profesa Mukandala kwa vyombo vya habari, wanafunzi waliokuwa katika safari hiyo ni wa kimataifa waliokuwa wakisoma shahada ya uzamili kupitia Programu ya Hisabati katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki. Miongoni mwa waliokufa katika ajali hiyo, wawili ni raia wa Malawi, Watanzania wawili, Mganda na Mzambia.

Watanzania waliokufa ni Nshaija Muganyizi, na Kassim Dadi, Wamalawi ni Chikondi Chasowa na Josephine Kaleso, Mganda ni Mubiru Patrick na Mzambia ni Chimuka Hamajata. Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa UDSM, Jackson Isidory, marehemu mmoja atazikwa kwao Bukoba, mwingine atapelekwa Uganda kama Idara ya Uhamiaji itaruhusu wengine wataletwa Dar es Salaam leo.

Kwa mujibu wa Isdory, wanafunzi watatu walioumia waletwa Dar es Salaam ili watibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Rose Mara, John Andonisye na Mwale Moses.  Basi la Taqwa lenye namba za usajili T 635 ABC aina ya Nissan Diesel lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Bujumbura Burundi liligongana na lori la Kampuni ya Bakhresa lenye namba za usajili RAB 255ACT lililokuwa likitoka Ngara kwenda Dar es Salaam. Magari hayo yaligongana Jumamosi saa nne asubuhi katika eneo la Lusahunga wilayani Biharamulo.

CHANZO HABARI LEO.

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI..AMEN.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s