KUTOKA CHUO CHA TAIFA ZANZIBAR(SUZA): KUADHIMISHA MIAKA 10 YA CHUO HICHO MWEZI HUU.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof.Idris Ahmada Rai akizindua CD ya Utafiti wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika Visiwa vya Zanzibar kwa Waandishi wa Habari katika hafla iliyofanyika Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar ( Suza ) Profesa Idris Ahmed Rai amesema, wakati umefika sasa Chuo hicho kuwa ni chuo chenye hadhi ya kimataifa ili kiweze kutambulika duniani kote . Aliyasema hayo leo huko katika uzinduzi wa sherehe za miaka kumi ya Chuo Kikuu cha Suza ambazo zinatarajia kufikia kilele chake siku ya tarehe 24 mwezi huu. Alifahamisha kuwa ukuwaji wa chuo hicho unatarajiwa kuwa katika awamu tofauti ambapo katika awamu ya kwanza, kunatarajiwa kuanzishwa skuli ambazo zinatokana na na idara au taasisi zilizopo hivi sasa ili kuweza kutoa fursa muhimu kwa skuli na idara zake mpya kuwa na uwezo mkubwa wa kukuza programu zake Alieleza kuwa chuo kikuu cha SUZA kinajipanga vyema kuisaidia serikali katika kufanikisha sera yake ya kukuza utalii kwa kuweza kusomesha utalii katika chuo hicho na skuli hiyo itaundwa kuwatayarisha vijana kuwa na ujuzi wa kazi katika sekta hii ili waweze kunufaika kiajira. Akifafanua azma ya chuo hicho Profesa Rai alisema kuwa, ni kukifanya chuo kua bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na chenye kutoa elimu yenye kiwango cha hali ya juu katika vigezo vya kimataifa. PICHA ZOTE NA Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s