KUTOKA TUMAINI IRINGA: Timu ya Soka ya Chuo Kikuu cha Tumaini -Iringa yapata kocha

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Tumaini Iringa Mussa Maundi akitoa maelekezo kwa wachezaji wa kikosi chake.

Mchezaji hatari wa kikosi cha Tumaini Iringa, Lazaro Mlyuka.

NA: LAZARO MLYUKA.

Timu ya mpira wa miguu ya chuo kikuu cha Tumaini Iringa imepata kocha atakayeweza  kuifua katika kujiandaa na mashindano ya VyuoVikuu maarufu kama TUSA yanayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu huko mkoani Tanga. Kocha huyo,Mussa Maundi, aliwahi kuifundisha timu ya Chuo mwaka 2004-2005 na kufanikiwa kuiletea mafanikio na heshima kubwa katika mashindano ya vyuo vikuu vya Afrika mashariki.

Aidha ana uzoefu wa kutosha katika tasnia hii ya soka hivyo kurudi kwake kuifundisha timu ya chuo kutasaidia timu kufanya vizuri katika mashindano yanayowakabili hapo baadae. Mbali na kuifundisha timu ya chuo, kocha huyo aliwahi pia kuzifundisha timu za Polisi na Lipuli zote za mkoani Iringa pamoja na timu ya mkoa wa Iringa (Mkwawa Heroes) kwa kipindi kirefu tu.

Baada ya kutambulishwa kwa wachezaji, Maundi alisema, “Naomba ushirikiano wenu wa dhati kwa yeyote mwenye nia ya kuipa heshima chuo, pia nidhamu ni jambo la kuzingatia sana kwenye mchezo wa soka japo muda tulionao ni mdogo lakini natarajia kuwafua vyema ili tuweze kufanya vizuri kwenye mashindano yanayotukabili”.

Naye mshauri  wa wanafunzi Mchungaji Osward Ndelwa, alimshukuru kocha huyo kwa nia yake ya dhati ya kutaka kuisadia timu ya chuo na kuwaomba wachezaji kutoa ushirikiano wao wa dhati kwa kocha huyo pamoja na kuonesha nidhamu ya hali ya juu katika mazoezi na mechi watakazocheza ili kuleta heshima katika  chuo chetu.

Pia nahodha wa timu hiyo George Kanju, aliwasihi na kuwahamasisha wachezaji wenzake kutii maagizo ya mwalimu huyo na kuzingatia mahudhurio ya mazoezi ili kufanikisha nia yao ya kufanya vizuri katika mashindano. Timu ya mpira wa miguu ya chuo kikuu cha Tumaini Iringa inaundwa na wachezaji ambao ni wanafunzi kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa tatu ambao wako katika mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo.

Katika mashindano hayo ya TUSA chuo cha Tumaini kinashikilia ubingwa katika mchezo wa  mpira wa wavu na mpira wa meza hivyo ni changamoto kwao kushinda michezo mingine kama mpira wa miguu, kikapu na pete. 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s