KUTOKA MZUMBE: WANAZUONI WAKUMBUSHWA KUSOMA VITABU.

Wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

WANAZUONI nchini wameshauriwa kujenga tabia ya kusoma vitabu ili kuwawezesha kujenga utamaduni wa kuandika vitabu vitakavyosaidia kurithisha vizazi vijavyo taaluma walizonazo kwa faida ya jamii na taifa kwa ujumla kama njia ya kusukuma gurudumu la maendeleo nchini.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa wakati akizindua kitabu cha Menejimenti ya Rasilimaliwatu kilichoandikwa na mmoja wa wanazuoni wa chuo hicho, Profesa Josephat Itika ambacho kitatumika kama kitabu cha rejea kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kitabu hicho kinajulikana kama ‘Fundamentals of Human Resources Management’.

“Tunamshukuru msomi mwenzetu ameweza kuandika kitabu hiki pamoja na kwamba ana majukumu mengi, lakini ameweza na hiyo inatoa fundisho kwetu sisi kama wanazuoni kuweza kuandika vitabu ili wanafunzi waweze kuwa na vitabu vingi na vinavyoendana na mazingira ya Kitanzania,” alisema Profesa Kuzilwa.

Alisema kitabu hicho amekiangalia kwa undani kinahusu Menejimenti ya Rasilimaliwatu na kina visa vya Afrika na Tanzania, kama inavyofahamika vitabu vingi vinavyotumika nchini vina hadhi ya kimagharibi hivyo kitabu hicho ni muhimu kwa wanafunzi, watumishi wa umma na kampuni binafsi kupata ujuzi.

Alisema kitabu hicho kimeandikwa kwa msaada wa miradi inayofadhiliwa na Shirika la Serikali ya Uholanzi (NOFIC) ambalo limekuwa likisaidia miradi mbalimbali chuoni hapo. Alisema Profesa Josephat Itika mbali na kuandika kitabu hicho, pia ameteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Taaluma na pia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimaliwatu, hivyo kazi aliyoifanya ni kazi kubwa sana ambayo inatakiwa kuigwa na kila mwanazuoni chuoni hapo na vyuo vingine nchini.

Mwandishi wa kitabu hicho, Profesa Josephat Itika, alisema kazi ya kuandika kitabu hicho cha Menejimenti ya Rasilimaliwatu ilikuwa ni kazi ngumu, lakini hatimaye aliweza kukikamilisha na sasa kimezinduliwa kwa ajili ya wanafunzi na watu walioko kazini wa taaluma hiyo.

Alisema changamoto iliyopo kwa wanazuoni waliopo nchini ni kuandika vitabu vingi ili wanafunzi waweze kutumia vitabu vyenye mazingira ya hapa nchini tofauti na ilivyo sasa vitabu vingi vinavyotumika vimeandikwa kwa mazingira ya nchi za Ulaya na maeneo mengine duniani.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Utawala na Fedha, Profesa Faustin Kamuzora alisema wanazuoni lazima wajenge tabia ya kuandika vitabu ili kuchangia wanafunzi na wasomi walioko makazini kuweza kupata ujuzi zaidi unaoendana na Tanzania kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya nchi.

“Nachukua fursa hii kuhamasisha wanazuoni nchini kuwa kazi ya kuandika vitabu inamwezesha mwandishi kama msomi kukumbukwa zaidi na vizazi hadi vizazi kwa kuwa binadamu huishi na kisha hufariki hivyo kupitia kazi hiyo majina yao hayatapotea yatakubukwa daima,” alisema Profesa Kamuzora.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s