KUTOKA SAUT: COMMUNITY DAY YAENDELEA LICHA YA MVUA KUBWA KUNYESHA..

Makamu mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino akifungua rasmi maonyesho hayo ya jumuiya ya wanaSAUT katika viwanja vya Raila Odinga leo hii. Padri Dr. Charles Kitima alisema kuwa wanafunzi na walimu wote wa SAUT ni lazima wazingatie taaluma bora kila siku na ni jukumu kwa mwanafunzi na mwalimu kuingia darasani na kutumia ipasavyo masaa matatu ya kipindi husika kila wiki, akizungumzia juu ya swala la wasomi kuitumikia jamii yao alisema kuwa wasomi wanatakiwa kuendeleza jamii kwa kuwa na malengo binafsi na malengo ya kuendeleza jamii kwani hakuna jamii yenye maendeleo bila ya wasomi hivyo wasomi wanamchango mkubwa wa kuiendeleza jamii. VC pia alizungumzia juu ya maamuzi ya uongozi wa chuo kuweka sheria juu ya mavazi na kusema kuwa sheria hiyo imeweka ili kujenga kizazi bora chenye heshima na kuthamini utu wake siku zijazo, na kusisitiza kuwa kwa mwanafunzi kuwepo chuoni hakumaanishi kuwa anajilea mwenyewe peke yake bali chuo pia kinahusika katika malezi hayo.

Kikundi cha sanaa cha SAUT (SAUT ARTS GROUP) kikitoa burudani katika maonyesho hayo.

Msanii mwenye kipaji kikubwa cha kuimba na kupiga gitaa Emmanuel Nyambita akitoa burudani ya aina yake katika ufunguzi wa maonyesho hayo.

Moot Court ya wanafunzi wa sheria nayo ilikuwa ni moja ya kivutio katika maonyesho hayo. Hapa kesi iliyokuwa inaendelea ni kesi ya ubakaji ya mtoto mdogo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s