KUTOKA SAUT: KITIVO CHA SHERIA CHAZINDUA JARIDA LA SHERIA (SAUT LAW JOURNAL) LEO ASUBUHI.

Kitivo cha sheria cha Chuo cha Mtakatifu Agustino kwa kushirikia na uongozi wa Chuo hicho leo kimezindua jarida maalum litakalo andika mambo mbalimbali ya kisheria hapa nchini kwa kupitia tafiti mbalimbali za wasomi zinazofanyika na wanataaluma hiyo.

Uzinduzi huo uliohudhuria na Madam Justice wa  Kanda ya Mwanza Aisheri Sumari akiwa ni mgeni rasmi ulihudhuria na mamia ya wanafunzi wa sheria kutoka chuoni hapo katika ukumbi wa M13wa chuo hicho. Wageni wengine waalikwa walikuwa ni Padri Dr. Charles Kitima, makamu mkuu wa chuo hicho, Balozi Prof. Mahalu, Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha chuo hicho Mr. Deodatus Kirangi, Prof. Christabella Joseph ambae ni Mhadhiri wa chuo hicho kitivo cha sheria pamoja na Sister Dr. Bandio Hellen, Director of Reserch and Publications wa chuo hicho.

Madam Justice wa Mahakama kuu kanda ya Mwanza Madam Aisheri Sumari(Wa tatu kulia), Prof. Christabella Joseph (wa kwanza kulia) na Sister Dr. Hellen Bandio anaefuata. Padri Dr. Charles Kitm (wa tatu kulia) Balozi Prof. Mahalu wa pili kulia na kulia kwa VC ni Mr. Kilangu wakiwa katika uzindizi huo wa jarida la sheria mapema leo asubuhi.

Padri Dr. Charles Kitima, makamu mkuu wa SAUT akitoa hotuba yake kweye uzinduzi huo. Aliipongeza department nzima ya kitivo cha sheria kwa juhudi kubwa za kutoa wanasheria bora SAUT, Kwani masomo ya vitendo na darasani yamekuwa yakiwapa uwezo mkubwa wanafunzi wa sheria kufanya vizuri katika tasnia hiyo. Akielezea historia ya Kitivo hicho Dr. Kitima alisema kuwa kitivo hicho kilianza na staff members watano na yeye akiwemo lakini kila mwaka imekuwa ikipata walimu wapya toka nje na ndani ya nchi. Akiwapongeza wahitimu wa batch ya kwanza wa kitivo hicho Dr. Kitima alisema kuwa wanafunzi 20 wa kitivo hicho wanaotunukiwa vyeti vyao kesho wamepata udhamini wa kusoma shahada zao ya pili katika chuo hicho.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jarida hilo Madam Justice wa mahakama kuu kanda ya Mwanza akizindua rasmi jarida hilo la watu wa sheria.

Wanafunzi hao wa sheria wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo wa jarida hilo.

Advertisements

2 responses to “KUTOKA SAUT: KITIVO CHA SHERIA CHAZINDUA JARIDA LA SHERIA (SAUT LAW JOURNAL) LEO ASUBUHI.

  1. “Askofu” Dr. Charles Kitima, makamu mkuu wa SAUT akitoa hotuba yake.

    Kwa jinsi ninavyofahamu Kitima hajawahi kuwa askofu verify the title before you post it

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s