KUTOKA IFM: MAHAFALI YA 37 YAFANYIKA IJUMAA, MKULO AKERWA NA WATAALAMU WA KIGENI NCHINI.

Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara,kutoka kushoto ni Huberth Assenga,Sisty Kimaro na Akim Joseph,wakipitia kitabu chenye majina ya wahitimu wa mahafali ya Thelathini na saba (37) ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) yaliyofanyika Dar es Salaam jana. (Picha na Yusuf Badi)

WAZIRI wa Fedha, Mustafa Mkulo amevitaka vyuo nchini kutoa mafunzo kwa vijana kwa kiwango cha kimataifa ili kuziba pengo la uhaba wa wataalamu na hatimaye kupunguza gharama za kupata wataalamu kutoka nje ya nchi.

Mkulo aliyasema hayo ijumaa jijini Dar es salaam katika mahafali ya 37 ya chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) ambapo wahitimu 2,482 walitunukiwa vyeti katika fani mbalimbali. “Serikali inafahamu uhaba wa wataalamu nchini ambao unasababisha baadhi ya Mashirika ya Serikali na watu binafsi kuendelea kuajiri wataalamu wa nje, ili kuziba pengo hili inatubidi tutoe mafunzo kwa kiwango cha kimataifa,” alisema.

Alisema viashiria mbalimbali vinaonesha kuwa Watanzania wengi sasa wanatambua umuhimu wa elimu kutokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo mbalimbali, hivyo wazazi na wahisani wataendelea kuwapeleka watoto wao katika vyuo hivyo endapo vitaendelea kutoa mafunzo yenye viwango vya kimataifa na yanayokidhi matakwa ya soko la ajira.

“Tafiti mbalimbali za wataalamu wa uchumi duniani zinaonyesha kuwa nchi ambazo uchumi wake umekuwa kwa kasi ni nchi ambazo zimewekeza zaidi kwenye rasilimali watu, hivyo kukua kwa uchumi wetu kutategemea hasa ni kiwango gani tumewekeza katika elimu” alisema.

Pia alikitaka chuo hicho kuendelea na mipango ya kuihusisha sekta binafsi katika miradi mingi ili kiepuke utegemezi wa ruzuku kutoka Hazina ambayo imekuwa haitoshelezi mahitaji ya maendeleo ya chuo. Aidha aliwataka wahitimu kuendelea kujifunza mbinu mpya za kuyakabili mabadiliko yanayotokana na utandawazi na kuwa waaminifu na waadilifu katika kusimamia fedha za waajiri wao sambamba na kujikinga na janga la ukimwi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Casmir Nyoni alisema wameanza kulipia fidia ya eneo la ekari 1,500 kwa ajili ya kuanzisha kampasi ya pili ya chuo hicho huko Msata Bagamoyo ili kukiwezesha kudahili wanafunzi wengi zaidi na hivyo kuliwezesha Taifa kupata wataalamu wengi zaidi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s