KUTOKA SUZA: SMZ yapania Chuo Kikuu Z’bar kiwe mfano Afrika.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inakusudia kukiendeleza Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) ili kiwe mfano katika ukanda wa Afrika Mashariki na bara lote la Afrika.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ofisini kwake migombani alipokutana na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idrisa Rai. Amesema inawezekana kwa chuo hicho kupata mafanikio makubwa kutokana na mipango yake imara ya kuimarisha miundombinu ya majengo pamoja na kuanzisha vitivo mbalimbali vya masomo yanayokwenda na wakati.

Ameuomba uongozi wa chuo hicho kufikiria pia kuanzisha kituo cha utafiti wa kilimo hasa kwa zao la karafuu ikizingatiwa kuwa hilo ni zao tegemeo katika uchumi wa Zanzibar. Aidha ameunga mkono malengo ya chuo hicho kuweka msisitizo katika taaluma ya habari na mawasiliano ICT kwani ina mchango mkubwa katika maendeleo ya sasa ya sayansi na teknolojia.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idrisa Rai amesema Chuo hicho kinakusudia kupanua huduma zake kwa kuingiza taaluma ambazo zitasaidia maendeleo ya jamii. Amezitaja baadhi ya taaluma hizo kuwa ni pamoja na utalii, kilimo, habari na mawasiliano, sambamba na kutoa mafunzo ya ngazi ya shahada ya pili na tatu kwa fani ya Kiswahili.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s