MAHAFALI YA SAUT YAFANA SIKU YA JANA.

Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT-Main Campus) jana kimefanya sherehe za mahafali ya kumi na tatu ambapo ambapo wahitimu 3035 walitunukiwa vyeti vya elimu ya cheti, stashahada, shahada pamoja na shahada ya uzamili huku wanawake katika idadi hiyo walikuwa ni 1262 sawa na 46% na wanaume 1634 sawa na 46% na zaidi ya watu 300 hawakuhitimu kutokana na sababu mbalimbali kubwa ni kufeli baadhi ya masomo hivyo kutakiwa kurudia.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa ni Mhashamu baba askofu wa jimbo kuu la Mwanza Jude Thadaeus Ruwa’ichi ambae pia ni Mkuu wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino anaemaliza muda wake mapema mwezi wa sita mwakani. Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na wageni wa serikali wa mkoa, wilaya, jaji mkuu wa mahakama kuu ya Mwanza, wakuu wa vyuo vishiriki vya SAUT, wahadhiri pamoja na wadau mbalimbali wa Chuo hicho.

Aidha akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu mkuu wa Chuo hicho Rev. Dr. Charles Kitima alisema kuwa kwa mara ya kwanza mahafali hayo yanatoa wahitimu wa shahada ya sheria na ugavi ambapo mafanikio yote ya chuo hicho mpaka kinafika hapo kilipo ni kutokana na ushirikiano mzuri kati ya walimu, wanafunzi pamoja na wazazi kufanay kazi kwa pamoja.

“Jamii inatarajia kuona matatizo yanapungua hapa nchini kwa kuwa wasomi wameongezekea hivyo wahitimu mnapaswa kulitumikia Taifa lenu kwa uadilifu na kwa uzalendo kwani kizazi chetu kimeshindwa kulitumikia Taifa na kuvunjo miko aliyoianzisha Mwalimu Nyerere” Alisema Dr. Kitima.

Dr. Kitima alimalizia kwa kusema kuwa Upungufu wa ajira unaolikabili Taifa na kutokana na kutokuwa na uchumi unaomilikiwa na wazawa wa nchi hii ambapo wanafunzi wa chuo hicho wamepata wafunzo ya kukabiliana na changamoto zote za mfumo wa ajira hapa nchi na ndio maana kila programu katika chuo hicho n lazima isome somo la ujasiriamali ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kutengeneza ajira binafsi.

Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino Jude Thadaeus Ruwa’ichi (wa mwisho) ambae pia ni mgeni rasmi katika mahafali hayo, wa tatu kutoka mwisho ni Makamu mkuu wa Chuo hicho Rev. Dr. Charles Kitima wakiingia katika mahafali hayo hapo jana.

Wageni meza kuu wakiwa tayari kwa kuimba nyimbo ya Taifa mara tu baada ya kuingia katika viwanja hivyo.

`

Eahitimu wa shahada ya Mawasiliano ya Umma wakivaa kofia kuashilia kutunukiwa shahada zao huku nyuso zao zikiwa na furaha.

Wahitimu wakiwa tayari kutunukiwa shahada zao.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s